23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wakazi Bughudadi Mbagala kupata maji ya uhakika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jumla ya wakazi 1,850 wa mtaa wa Bughudadi, kata ya Mbagala, Jijini Dar es Salaam wanatarajiwa kunufaika na huduma ya majisafi kupitia utekelezaji wa mradi wa maji Kizinga – Bughudadi.

Mradi huo unaotekelezwa kwa kutumia fedha za ndani unatekelezwa kwa lengo la kusogeza mtandao wa maji kwa wananchi wa mtaa wa Bughudadi.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi huu, Msimamizi wa mradi, Mhandisi Azizi Namanga, amesema kuwa mradi umehusisha ulazaji wa mabomba ya ukubwa wa inchi 3, 2 na 1.5 kwenye umbali kilomita 1.8.

Amesema pia kuwa mradi huu ni mahususi kwa ajili ya kusogeza huduma ya maji kwenye mtaa wa Bughudadi kutoka kwenye mtaa wa Kizinga.

“Tumeamua kutekeleza zoezi hili baada ya kuharibika kwa miundombinu ya maji iliyokuwepo kwenye mtaa wa Bughudadi,” ameeleza.

“Pia mradi umejenga vizimba viwili vya kuchotea maji kwenye mtaa wa Bughudadi ili kuwezesha wananchi kupata maji kwa urahisi,” amesema Mhandisi.

Kwa sasa kazi inayoendelea kwenye eneo la mradi ni pamoja na uchimbaji wa mtaro kwa kuweka mabomba ya mtandao wa maji.

Mhandisi Namanga amebainisha kuwa mradi unatarajiwa kukamilika tarehe 29 Desemba na utakabidhiwa kwa ofisi ya Mkoa wa kihuduma Mbagala kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Bughudadi, Seif Mohammed ameipongeza DAWASA kwa jitihada za kufikisha huduma ya maji kwenye mtaa wake.

Amesema kuwa kwa muda mrefu wakazi wa mtaa huo hawakua hawapati maji kutokana na miundombinu ya maji kuharibiwa.

“Huu mradi utasaidia sana kuondoa kero ya ukosefu wa maji kwa wananchi wa mtaa wa Bughudadi.

“Tunaomba kazi inayoendelea ikamilike ndani ya muda ili wananchi waweze kufurahia huduma,” amesema Mohammed.

Mkazi wa mtaa wa Bughudadi, Mariam Peter ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi wa maji Bughudadi utawapa nafuu ya kupata maji kwa wepesi baada ya kukosa maji kwa muda mrefu.

“Tunashukuru maana kukamilika kwa mradi huu utatupa uhakika wa kupata maji bila changamoto,” ameeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles