23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

WAJASIRIAMALI TAFOPA WATAKA MAENEO YA VIWANDA

Wazalishaji wadogo wa chakula wakiwa kazini
Wazalishaji wadogo wa chakula wakiwa kazini

Na FERDNANDA MBAMILA, DAR ES SALAAM

TAASISI  isiyo ya kiserikali inayojihusisha na usindikaji wa vyakula  mbalimbali nchini  ya Tanzania Food Processing  Association (Tafopa), imeendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo ili kufikia lengo wanalotarajia.

Lengo la Taasisi hii ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo ili kuwakomboa katika suala zima la utengenezaji wa bidhaa mbalimbali  katika mazingira yaliyo salama.

Pia taasisi hiyo imeiomba Serikali iwasaidia kwa kuwatengea maeneo maalumu ya viwanda ambayo yatakuwa yamesheheni huduma zote za kijamii na zinazohitajika katika viwanda  hususani umeme na maji.

Hii inatokana na kuwepo kwa wajasiriamali walio wengi kuwa na taaluma ya elimu ya kutosha juu ya usindikaji wa bidhaa, lakini kinachowakwamisha  na kushindwa kuendelea ni kukosa wadau wa kuwawezesha  ili kufikia malengo waliyoyakusudia.

Moja kati ya changamoto  inayowakumba wajasiriamali hao  ni kukosa vifaa vya kusindikia bidhaa hizo ambapo wangeweza kupata wadau watakaoweza kuwasaidia  kwa wakati na hivyo wangefika mahali sahihi katika suala zima la usindikaji wa vyakula.

Lakini changamoto hiyo imegeuka kuwa  chungu zaidi baina yao  kwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira hafifu ambapo kama msindikaji unatakiwa kuwa na sehemu maalumu kwa ajili ya kufanyia shughuli hizo na si katika makazi ya kuishi.

Ingawa Tanzania ya sasa imeanza kuwa na uwepo mwingi wa  viwanda  mbalimbali vya uchakataji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, lakini hakuna mipango thabiti   kwao ya kuwasaidia katika zoezi zima.

Mwenyekiti  wa  Chama cha Usindikaji wa vyakula nchini, Suzy Laiza, anasema  wao kama Taasisi ya Mayoda  wamewawezesha wasindikaji wadogo  ili waweze kupata maeneo maalumu ya  usindikaji wa bidhaa hizo.

Anasema  hadi sasa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini  (Sido), wameweza kutuunga mkono kwa kuwapa mafunzo ya usindikaji wa vyakula kwa wajasiriamali wadogo zaidi 600 katika taasisi hiyo ili kuwasaidia wajasiriamali hao kufikia malengo yao.

“Hapo awali wasindikaji walikuwa wanafanya shughuli zao wakiwa katika majumba  yao kwa kukosa  sehemu maalumu ya kuzalisha  bidhaa  hizo, kwani kama wana ujuzi na maarifa ya kutosha na uwezo wa kuweza kuzalisha  na wameonyesha moyo  kwanini  wasisaidiwe!”anasema Laiza.

Tuliona ni vyema zaidi kwa  kupitia mkutano  tulioufanya Novemba 13, mwaka jana wa kuwakutanisha  wadau  wa sekta mbalimbali kwa pamoja ili kuinua na kuviendeleza viwanda  vyetu hapa nchini,  lengo letu lilikuwa  kuwawezesha wasindikaji wadogo  nchini.

“Si kwamba tumetosheka na mafunzo pekee bali tunaomba na tunazidi kuomba taasisi mbalimbali ili kutuunga mkono kwa suala la viwanda ili kukuza uchumi wan chi.

“Kwa hiyo kwa yeyote atakayeguswa katika hali, basi tunawakaribisha ili kutoa hata mchango wa  mawazo kwani kwetu ni faida tosha.

Ingawa wamepata mafunzo  ya kutosha ya usindikaji wa vyakula mbalimbali, lakini  bado wanakabiliwa na changamoto ya kukosa  maeneo maalumu ya kusindika malighafi hizo, ndio maana tuliweza kuwaalika wadau hao ili waweze kutusaidia  kwa hali yoyote ile ili tuweze kuondokana na tatizo hili ambalo limekuwa ni kikwazo kwa wasindikaji walio wengi nchini,” anasema Laiza.

Mafunzo na mawazo ya wadau wa taasisi mbalimbali hayatoshi pekee kuwafikisha mahali wanapostahiki kufika, bali kubwa zaidi ni watengewe maeneo maalumu kwa ajili ya viwanda ambayo yatakuwa yamesheheni huduma za kijamii katika kiwanda.

Hamasa iliyotolewa na taasisi hiyo ya kuitaka Serikali na wadau wa taasisi mbalimbali nchini kuweza kutoa mchango wao iweze kuzaa matunda ifikapo mwaka huu ili kuviinua viwanda vyetu na kufikia mahali tunapostahili katika kufanikisha lengo letu, Watanzania kuwa na Tanzania ya viwanda kama kauli na rai ya Rais Dk. Magufuli  inavyosema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles