Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Serikali imelitaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha linatoahuduma bora na za viwango kwa Watanzania mara baada ya mradi waujenzi wa reli ya kisasa ya (SGR) sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogorokukamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, kufuatia wasiwasi wa wananchi kuhusu masuala yamiundombinu ya umeme wa reli hiyo ambapo pamoja na mambo mengine Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali kupitia Shirika hilo imejidhatitikwa kuweka vyanzo vya umeme vitatu tofuati na vichwa vya kutumiadizeli ili kutatua changamoto zozote zitakazojitokeza.
“Napenda kuwatoa wasiwasi Watanzania kuwa Serikali kupitia TRCimejipanga sawasawa kuhakikisha umeme hautakuwa changamoto wakatiwa uendeshaji wa treni hii,” amesema Waitara.
Aidha, Waitara amelitaka Shirika hilo kujipanga na kuhakikisha kuwawataalam wazawa waliopata ujuzi kwenye mradi huo wanatumikaipasavyo mara baada ya mradi kukamilika.
Waitara, amelipongeza Shirika hilo kwa kuajiri watalaam na kusimamiavizuri mradi huo kwa sehemu ya Makutupora hadi Morogoro na Morogorohadi Dar es Salaam.
Naibu Waziri Waitara amemhakikishia Mkurugenzi wa TRC kuwa Serikaliitaendelea kuhakikisha inatoa fedha ili mradi uweze kukamilika na Watanzania wafaidi matunda ya Serikali yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Masanja Kadogosa,amesema kuwa TRC imeshaajiri wahandisi zaidi ya 200 ambao kwa sasa wamewekwa kwenye miradi ili kupata ujuzi na uendeshaji wa reli hiyo yakisasa mradi utakapokamilika.
Kuhusu upatikanaji wa mabehewa Kadogosa amefafanua kuwa tayari manunuzi yako kwenye hatua nzuri na vichwa vitawasili mapema Julai, mwaka huu na majaribio ya treni ya kwanza kwa sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro yatafanyika Agosti, mwaka huu.
Naye, Meneja Mradi wa sehemu ya Morogoro – Dar es Salaam, Mhandisi Simon Mmbaga, amesema mradi huo kwa sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro umeshakamilika na asilimia zaidi ya 93 na kazi zinazoendelea kukamilishwa ni pamoja na kuunganisha mifumo mbalimbali katika vituo.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amekamilisha ziarayake ya siku mbili ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa reli yaKisasa ya SGR kwa sehemu ya Makutupora hadi Morogoro na Morogoro hadi Dar es Salaam.