26.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Waislamu watakiwa kujiandaa Uchaguzi Mkuu 2015

Sheikh Rajabu Katimba
Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba

Na Asifiwe George, Dar es Salaam

WAUMINI wa dini ya Kiislamu nchini wametakiwa kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kujiandikisha upya katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaloanza Septemba, mwaka huu.

Amesema kufanya hivyo kutawasaidia kufanya maamuzi sahihi dhidi ya viongozi wanaowakwamisha kwa kuwaadhibu kupitia masanduku ya kura.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam juzi katika Baraza la Idd, lililofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga na Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba, ambaye alimtaka kila Mwislamu nchini kuhakikisha anajiandikisha.

Alisema hatua ya kujiandikisha kwenye daftari hilo ni hatua moja ya maandalizi ya kushiriki vyema kwa kufanya tafakuri kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Sheikh Katimba alipinga hatua ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa na ahadi nyingi, ikiwemo matumizi ya vitambulisho vya Taifa katika uchaguzi, lakini imeshindwa kufanya hivyo.

“Tulifuatilia suala hilo katika viongozi wa Tume na tuliwaulizia suala hilo, lakini walijibu kwamba wataandikisha upya majina katika Daftari la kudumu la wapiga kura na litaanza rasmi Septemba, mwaka huu,” alisema Sheikh Katimba.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Umoja wa Shule za Kiislamu, Hassan Saiboko, alisema kuna dhuluma inaendelea kwa wanafunzi wa dini ya Kiislamu, hasa katika masomo ya kidini.

Alisema masomo ya dini kwa sasa hayahesabiwi kwa wanafunzi wa kidato cha sita, hali inayosababisha wengine kushindwa kufikia malengo kutokana na somo hilo kutoingizwa katika alama na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

“Kutokana na hali hii, tunaiomba Serikali itazame suala hilo ili masomo ya dini yaweze kurudishwa na kutolewa alama kwa lengo la kukuza watu wengi kiimani. Wanafunzi wa Kiislamu wasikate tama, waendelee kusoma somo hilo kwa umakini zaidi, kwani ni faida katika maisha yao,” alisema Saiboko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles