32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wahusika taa katika daraja la kituo cha mwendokasi Morocco zimesahaulika

Na Juliana Gatawa

NDUGU Mhariri nawasilisha maoni yangu kuhusu kero hii ambayo nimekuwa nayo kwa kipindi kirefu.

Wakati usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaama maarufu kama mwendokasi,miaka kadhaa iliyopita kila mmoja wetu alikuwa akitamani kutumia usafiri huu.

Hiyo ilitokana na kuwapo kwa huduma nzuri na rafiki kwa abiria wote waliokuwa wakitumia usafiri huo unaoratibiwa na UDART.

Hata hivyo, ndugu mhariri pamoja na kuwapo kwa changamoto nyingi zinazokabili aina hii ya usafiri lakini nalazimika kutoa maoni yangu haya kutokana na changamoto kubwa iliyokuwepo hasa kwenye maeneo ya vivuko hususan eneo la Kinondoni Morocco.

Ndugu mhariri zamani ulipokuwa ukishuka kituo cga mwendokasi cha Morocco kisha kupandisha ngazi zilizko kwenye daraja liloko katika eneo hilo kulikuwa na taa zilizosaidia abiria waliokuwa wakitumia daraja hilo kuvuka bila wasiwasi kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Kinachosikitisha kwa sasa nikuona eneo hilo likiwa halina taa tena, kwa maneno mengine ni giza jambpo ambalo linatoa shangamoto kwa sisi abiri tunaotumia daraja hilo.

Hivyo, kupitia barua hii naomba kuzikumbusha mamlaka husika ziweze kutazama eneo hilo nakuweka miundombinu vizuri kama ilivyokuwa awali.

Kwani eneo hilo kukaa bila mwanga ndiko kunachochea vijana wasiowaaminifu kufanya vitendo visivyofaa ikiwamo kuandika lugha za matusi katika kuta za daraja hilo na hata wakati mwingine kukojoa hatua inayosababisha uchafu. Naomba kuwasilisha.

Mwandishi wa barua hii ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles