26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wa Ngorongoro kuhamia Msomera wakati wowote- Dk . Chana

Na Mwandishi wa NCAA, Msomera Tanga

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana ameeleza kuwa wakati wowote kuanzia sasa wananchi waishio katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wataanza kuhamia katika makazi mapya yaliyopo Kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Balozi Dk. Chana ametoa kauli hiyo Juni 9, 2022 alipofanya ziara ya kukagua hali ya utayari wa miundombinu ya makazi; maji, umeme, madarasa ya shule za msingi na sekondari, zahanati, majosho kwa ajili ya mifugo na barabara katika Kijiji hicho.

“Tumekuja kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa makazi, na huduma za kijamii kwa wananchi watakaohamia hapa. Nimeridhika sehemu kubwa ya miundombinu imekamilika, muda wowote kuanzia sasa wanangorongoro waliojiandikisha kwa hiari watahamia hapa kuendelea na maisha ili kupisha shughuli za Uhifadhi ndani ya eneo,” amefafanua Balozi Dk. Chana.

Ameeleza kuwa pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa nyumba 103 na huduma zingine za kijamii, Serikali inajipanga kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za makazi 400 kwa ajili ya kuwezesha wananchi wanaoendelea kujiandikisha kwa hiari kuhamia Msomera.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima ameleeza kuwa mkoa huo umeshaandaa mazingira ya kuwapokea wananchi wa Ngorongoro, hali ya kiusalama iko shwari na tayari vyumba saba vya madarasa, Maabara, Bweni na majosho kwa ajili ya mifugo yamekamilika sambamba na usambazaji wa huduma za maji, umeme na mawasiliano ya barabara.

Akiwa katika ziara ya Mhe Waziri, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ameeleza kuwa uongozi wa mkoa wa Arusha kuratibu zoezi la kuandikisha wananchi wanaotaka kuhama kwa hiyari na kaya zilizokwisha jiandikisha Serikali imeshapanga utaratibu wa kuwahamisha muda wowote kuanzia sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles