Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepitisha majina ya wagombea ubunge wa chama hicho katika mikoa mbalimbali chini ya mwamvuli wa Ukawa.
Katika uteuzi huo, baadhi ya wanasiasa na wanahabari wamefanikiwa kupenya katika chekeche la mchujo wa chama hicho na kufanikiwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika, iliwataja wanachama mbalimbali walioteuliwa na vikao vya maamuzi.
Mara
Katika majimbo ya Mkoa wa Mara walioteuliwa na majimbo yao katika mabano ni Steven Owawa (Rorya),  Esther Matiko(Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Zakaria Chiragwile (Musoma Vijijini) na  Yusuph Kazi (Butiama).
Wengine ni aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kupitia CCM, aliyejiunga na Chadema hivi karibuni, Esther Bulaya (Bunda Mjini), Â Harun Chiroko (Mwibara), Vicent Nyerere (Musoma Mjini) na Suleiman Daudi (Bunda Vijijini).
Simiyu
Katika majimbo ya Mkoa wa Simiyu walioteuliwa ni Godwin Simba (Bariadi), Abdalah Patel (Maswa Magharibi),  Sylvester Kasulumbayi (Maswa Mashariki),  Masanja Manani (Kisesa), Meshack Opulukwa (Meatu) na Martine Magile (Itilima).
Shinyanga
Wanachama walioteliwa ni Paulo Malaika (Msalala),  James Lembeli ( (Kahama Mjini),  Simon Isaya (Ushetu), Patroas Paschalk (Shinyanga Mjini) na Fred Mpendazoe (Kishapu).
Mwanza
Walioteuliwa ni Joseph Mkundi (Ukerewe), Kalwinzi Ngongoseke (Magu), Ezekia Wenje (Nyamagana), Martine Kaswahili (Buchosa), Hamis Tabasamu (Sengerema), Highness Kiwia (Ilemela) na Leonidas Kondela (Misungwi)
Geita
Mkoa wa Geita Profesa  Kulikoyela Kahigi (Bukombe), Alphonce Mawazo (Busanda),  George Mabula (Nyang’wale),  Dk Benedict Lukanima (Chato) na Nicodemus Maganga (Mbogwe).
Kagera
Mkao wa Kagera ni Prince Rwazo (Karagwe), Benedict Mtungirehi (Kyerwa), Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) Ansbert Ngurumo (Muleba Kaskazini), Â Alistides Kashasila (Muleba Kusini) na Dk. Anthony Mbassa (Biharamulo).
Mbeya
Wagombea waliopitishwa ni Njelu Kasaka (Lupa), Mpoki Mwankusye (Songwe), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Abraham Mwanyamaki (Kyela), John Mwambigija (Rungwe), Boniphace Mwamukusi (Busokelo), Paschal Haonga (Mbozi), David Silinde (Momba), Adam Nzela (Mbeya Vijijini), Frank Mwakajoka (Tunduma) na Fanuel Mkisi (Viwawa).
Iringa
Waliopitishwa ni Patrick Ole Sosopi  (Isimani), Mussa Mdede (Kalenga),  Jumanne Makonda (Mufindi Kaskazini), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Brian Kikoti (Kilolo) na Wille Mungai (Mafinga Mjini.
Njombe
Katika Mkoa wa Njombe ni Emmanuel Masonga (Njombe Kusini),  Edwin Swale(Lupembe), Dismas Luhwago (Wanging’ombe), Jackosn Mogela (Makete), Athromeo Mkinga (Ludewa), na Oraph Mhema (Makambako).
Rukwa
Waliopitishwa Mkoa wa Rukwa ni Alfred Sotoka (Nkasi Kusini),  Daniel Ngogo (Kwela), Kessy Soud (Nkasi Kaskazini), Sadrick Malila (Sumbawanga Mjini) na Victor Mateni (Kalambo).
Tanga
Waliopitishwa Mkoa wa Tanga ni Jeradi Mrema (Kilindi), (Muheza), Ernest Msingwa ( Korogwe) na Emmanuel Kimea (Korogwe Vijijini).
Kilimanjaro
Katika Mkoa wa Kilimanjaro waliopitishwa kugombea ubunge ni Joseph Selasini (Rombo),  Christopher Mbajo (Same Magharibi), Nagenjwa Kaboyoka (Same Mashariki) Jafary Michael (Moshi Mjini),  Freeman Mbowe (Hai) na Godwin Mollel (Siha).
Mkoa wa Arusha ni Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Gibson Mesiyeki (Arumeru Magharibi), Godbless Lema (Arusha Mjini), Onesmo Ole Nangole (Longido) Julius Kalanga (Monduli), Wille Qambalo, (Karatu) na Elias Ngorisa (Ngorongoro).
Manyara
waliopitisha na chama hicho ni James Millya (Simanjiro), Mikel Aweda (Mbulu Vijijini), Magoma Derick (Hanang’), Pauline Gekul (Babati Mjini), Laurent Tarra (Babati Vijijini), Kidawa Athumani (Kiteto) na Paulo Sulle (Mbulu Mjini).
Dar es Salaam             Â
Waliopitishwa Mkoa wa Dar es Salaam   ni  Saed Kubenea (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga), Muslim Hassanali (Ilala) na John Mnyika (Kibamba).
Pwani
Kwa upande wa majimbo ya Mkoa wa Pwani ni Mathayo Torongey (Chalinze), Michael Mtaly (Kibaha Mjini)Â na Editha Babbeiya (Kibaha Vijijini).
Morogoro
Walioteuliwa Mkoa wa Morogoro ni Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay (Mikumi), David Lugakingira (Morogoro Kusini), Peter Lijualikali (Kilombero), Suzan Kiwanga (Mlimba), Oswald Mlay (Mvomero), Alphonce Mbassa (Ulanga Magharibi), Pancras Kongoli (Ulanga Mashariki) na Marcossy Albanie(Morogoro Mjini).
Dodoma
Waliopitishwa Mkoa wa Dodoma ni Esau Ngombei (Kongwa), Benson Kigaila (Dodoma Mjini), Mathias Lyamunda (Bahi) na John Chogongo (Chilonwa).
Singida     Â
Waliopitishwa ni Jesca Kishoa (Iramba Magharibi), Oscar Kapalale (Mkalama), Davis Jumbe (Singida Kaskazini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Marco Allute (Singida Magharibi), Lupaa Donald (Manyoni Magharibi) na Allute Emmanuel (Manyoni Mashariki).
Tabora
Kwa majimbo ya Mkoa wa Tabora waliopitishwa ni Charles Mabula (Nzega Mjini), Ngwigulu Kube (Igunga), Samweli Ntakamalenga (Urambo), mbunge anayemaliza muda wake kupitia CCM, Said Nkumba (Sikonge), Deus Ngerere (Ulyankulu) na Ally Nguzo (Manonga).
Katavi
Waliopitishwa Mkoa wa Katavi ni Jonas Kalinde(Mpanda Mjini), Mussa Masanja (Mpanda Vijijini), George Sambwe (Katavi), Â Gerald Kitabu (Nsimbo) na Laurent Mangweshi (Kavuu).
Kigoma
Waliopitishwa Mkoa wa Kigoma ni Dk. Yared Fubusa(Kigoma Kaskazini) na Daniel Lumenyela(Kigoma Mjini).
Ruvuma
Waliopitishwa Ruvuma     ni Elasmo Mwingira (Peramiho) na Cutherth Ngwata (Mbinga Magharibi), Edwin Kitanda (Mbinga Vijijini), John Fuime (Songea Mjini) na Edson Mbogoro(Madaba).
Kutokana na uteuzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo wa Chadema Bara, John Mnyika orodha ya majimbo yaliyobaki itatolewa baada ya kukamilika kwa mashauriano katika vikao vya Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA).