29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wafungwa wa wanyimwa chanjo ya corona Israel

Palestina

Chama cha Wafungwa wa Palestina kimetaka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kuweka shinikizo kwa utawala wa Tel Aviv kuwaruhusu Wapalestina katika magereza ya Israel kupewa chanjo dhidi ya corona.

Chama cha Wafungwa wa Palestina kilifanya mkutano na waandishi wa habari mbele ya jengo la Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika Ukanda wa Gaza.

Ahmed al-Mudellel, Afisa wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu, alizungumza kwa niaba ya Chama na kusema,

“Kuenea kwa haraka kwa janga la Covid-19 katika magereza kumesababisha hofu kubwa na wasiwasi kwa maisha ya wafungwa,”.

Mudellel amesema kuwa hali ya kiafya ya wafungwa wa Kipalestina katika magereza ya Israeli iko hatarini kutokana na janga hilo na kwamba Israel inakataa kuwapa chanjo wafungwa wa Palestina, na akautaka utawala wa Palestina “kupeleka suala hilo katika ngazi za kimataifa.”

Mudellel pia alitoa wito kwa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) “Kuweka shinikizo kwa Israeli kuruhusu matibabu na chanjo kutumika katika magereza,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles