32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wafungwa Butimba wamlipua Askari Magereza kwa Magufuli, atoa tamko

Anna Potinus

Wafungwa katika gereza la Butimba jijini Mwanza, wametoa kero zao ambapo wamewatuhumu baadhi ya askari magereza kufanya mambo yasiyostahili ikiwamo kunyang’anywa vitu vyao.

Kero hizo wamezitoa leo Jumanne Julai 16, gerezani hapo mbele ya Rais John Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza na kuzungumza nao.

Mmoja wa wafungwa anayetumikia kifungo cha miaka 30, Kalikenya Nyamboge, amemtuhumu Ofisa Usalama gerezani hapo kuwapa wafungwa simu halafu zikikamatwa wananyan’ganywa vitu vyao walivyo navyo lakini hadi leo hajafanywa kitu chochote.

“Mheshimiwa rais, huyu ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakiwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru.

“Sasa hivi Jenerali Kamishna ametuletea daktari msomi na alivyofika vifo ndiyo vimepungua maana walikua wakikuchoma sindano wanakuua.

“Na si mara ya kwanza wao kuua mimi nilikuwa nimepanga nikitoka nije kukwambia na nikitoka nitakuletea mambo yote yanayotokea huku lakini huyu usimuache maana kwa Mwenyezi Mungu utakua umeandika maelezo ya mauji,” amesema Nyamboge.

Kwa upande wake aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mbugani, Hashimu Kijuu, amesema yeye yuko gerezani hapo kwa kupewa kesi ya utakatishaji baada ya kuuza shamba lake huku askari mmoja aliyemtaja kwa jina la Sangali akimwambia ataozea jela.

“Mimi niliuza shamba langu lililopo Kisesa jijini Mwanza lakini matokeo yake Sangali aliniambia nitakaa jela hadi nitakapokuta mke wangu ameolewa, sasa ni maneno gani hayo,” amesema Kijuu.

Naye mfungwa mwingine Kulwa Alphonce, alikamatwa mwaka 2017 akiwa na mafuta ya dizeli akapelekwa Kituo cha Nyegezi askari wakamuomba Sh milioni moja, akawaambia ana 200,000 tu ambayo walikataa kisha baadaye wakampeleka ‘central’ baada ya hapo akafunguliwa kesi ya mauaji.

Aidha, mfungwa mwingine Shukrani Masegenya, alimuomba Rais Magufuli kuwapunguzia adhabu ya vifungo ili wakatumie ujuzi wao wanaofundishwa nje.

“Pamoja na kufanya kazi na kufundishwa stadi za kazi tunaomba utusaidie kuna watu tumefungwa miaka 30 wengine maisha hivyo tunaomba utupunguzie vifungo maana tunafundishwa hizo stadi za kazi wakati maisha yetu yanaishia humu ndani, tunatamani tukitoka tukatumie hizo stadi na tuwe vioo vya jamii huko nje,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles