26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

WAFUKUZWA KAZI KWA ULEVI, UBADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA

Na IBRAHIM YASSIN- ILEJE

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, imewafukuza kazi watendaji wawili akiwamo Ofisa ugavi, Joseph Murwa kwa ubadhirifu na ulevi kazini.

Watumishi wengine wawili wamepewa onyo kali.

Azungumza jana kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ubatizo Songa, alisema wameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kwa matendo yao.

Mwingine ni Alfred Mulala, aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Lubanda, akituhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma Sh milioni saba.

Mwenyekiti huyo alisema baada ya uchunguzi watumishi hao wamebainika kufanya makosa hayo kwa nyakati tofauti.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Ileje, Haji Mnasi, alisema ofisa ugavi alikutwa na pombe ofisini, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za utumishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles