26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

WACHUMBA WATUPWA JELA KWA WIZI

Na CAROLINE CHALE Na MAMII MSHANA (TUDARCO)- DAR ES SALAAM

WACHUMBA wawili jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh 100,000 na fidia ya Sh 300,000 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa mkoba kanisani.

Wachumba hao, Ayoub Sanga na Naphaife Kainga (19) wote ni wafanyabiashara na wakazi wa Ubungo Riverside jijini Dar es Salaam.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni na Hakimu, Ester Kihiyo baada ya watuhumiwa hao kukiri kosa lao.

“Ninawahukumu kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh 100,000 pamoja na kulipa fidia ya Sh 300,000 ili iwe onyo na fundisho kwa wote wenye tabia ya wizi kama ninyi hasa kwenye nyumba za ibada,” alidai Hakimu Kihiyo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuiba vitu hivyo ambavyo ni mkoba wenye fedha taslimu Sh 150,000 na simu tatu za Tecno, Huawei na Sumsung ndani ya Kanisa la T.A.G lililopo maeneo ya Kinondoni Biafra, mali ya Dorice Makenzi jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles