30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wachina watatu washatakiwa Kenya kwa rushwa

NAIROBI, KENYA

Raia watatu wa China wanaofanya kazi na reli mpya nchini Kenya (SRG) wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kujaribu kutoa rushwa.

Hii ni baada ya mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya kuidhinisha tume ya kupambana na ufisadi kuwafungulia mashtaka raia hao watatu wa China.

Li Gen, anayesimamia usafiri, Li Xiaou meneja wa ulinzi na Sun Xin ambaye ni mfanyakazi watafunguliwa mashtaka ya kujaribu kuwahonga maafisa waliokuwa wanachunguza sakata ya wizi wa pesa zinazotokana na mauzo ya tiketi.

Watatu hao wanaripotiwa kujaribu kuwahonga maafisa wa uchunguzi shilingi 500,000 za Kenya au dola elfu Tano.

Walikamatwa Ijumaa na maaafisa kutoka tume ya kupambana na ufisadi (EACC).

Ukizungumzia suala hilo ubalozi wa China mjini Nairobi kupitia mkurugenzi wake wa mawasiliano Zhang Gang alisema ubalozi unaheshimu uchunguzi unaofanywa na mamlaka za Kenya kuambatana na sheria za nchi hiyo.

Watatu hao hufanya kazi na kampuni ya China Roads and Bridge Corporation (CRBC) katika kituo cha treni cha Mombasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles