27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji wakiri Lugalo Open 2021 ilikuwa moto

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

BAADHI ya wachezaji wa Gofu walioshiriki shindano la Lugalo Open 2021 wamekiri kuwa mchuano ulikuwa mkali kutokana na kila mshiriki kuonesha kiwango bora.

Shindano hilo lililofanyika kwa siku tatu, likishirikisha wachezaji wa kulipwa na ridhaa zaidi ya 100 kutoka klabu mbalimbali, limehitimishwa jana kwa halfa ya utoaji zawadi iliyofanyika kwenye viwanja vya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Mshindi upande wa watoto, akipokea zawadi ya baiskeli kutoka kwa Mnadhimu wa JWTZ, Luteni Generali Mathew Mkingule.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi wa jumla, mchezaji Victor Joseph kutoka Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana, amesema pamoja na kuibuka kidedea lakini alipata upinzani mkali.

Victor ambaye ameshinda kwa mikwaju 150, amewataja wachezaji aliochuana nao vikali kuwa ni Ally Mchalo wa TPC ambaye amepiga mikwaju 154 na Malius Kajuna wa Lugalo mikwaju 158.

“Napenda kuushukuru uongozi wa Lugalo kwa kuandaa mashindano haya. Pia napenda kuwashukuru wachezaji wenzangu Ally Mchalo, Malius na Isihaka kwa ‘challange’ niliyoipata,” amesema Victor.

Kwa upande wake Peter Elias ambaye ni mshindi wa kwanza wa ‘division’ C , amesema uwepo wa jua kali imekuwa changamoto kwao kwani walikuwa wanachoka mapemba, lakini walipambana hadi mwisho.

Pia ameeleza kuwa mwaka huu kumekuwa na mashindano mengi na yaliyowajenga zaidi na kuwafanya bora.

Wageni waliohudhuria hafla ya utoaji wa zawadi za Lugalo Open 2021

Washindi wengine, kundi A ni Jyten Lavinga, aliyefungana na Michael Masawe kwa mikwaju 146, kundi B Lunacho Kigome wa Lugalo aliyepiga mikwaju 148, akifuatiwa na Khalid Shemndolwa kwa mikwaju 148.

Kundi C mshindi ni Peter Elias aliyepiga mikwaju 145, akifuatiwa na Amiri Kangajaka mikwaju 146.

Kwa upande wa wanawake Angel Eaton aliibuka kidedea kwa mikwaju 165, wa pili ni Joyce Warega mikwaju 146, namba tatu Zahara Shemndolwa mikwaju 150.

Kwa wanaume (seniors), mshindi ni Dk. Edmundi Shemndolwa kwa mikwaju 147, akifuatiwa na Gulam Dewji mikwaju 151. Watoto mshindi ni Ally Said mikwaju 68, wa pili ni Uzwaifa Suleiman Mikwaju 70.

Dk. Edmundi Shemndolwa (kushoto), akipokea zawadi kutoka Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Generali Mathew Mkingule
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles