27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wachezaji Simba wako tayari kuhesabika Agosti 23

Na Mwandihi Wetu, Mtanzania Digital

Wachezaji wa Klabu ya Simba Sc hii leo Agost 8, 2022 wakiwa katika maandalizi ya mwisho kuelekea tamasha kubwa la SIMBA DAY ambapo inatarajiwa kucheza dhidi ya Mabingwa wa soka ligi kuu ya Ethiopia klabu ya St. George Sc wametumia muda wao kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la Sensa la Agosti 23, 2022.

Wachezaji hao wakiongozwa na Nahodha John Bocco, wameungana na Shomari Kapombe, Aishi Manula, Erasto Nyoni na wazawa wengine kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wako tayari kuhesabiwa.

“Sisi wachezaji wa Simba Sc tunapenda kuwahamasisha watanzania wajitokeze kuhesabiwa kwani ni muhimu kwa maendeleo na mipango ya nchi yetu, tumuunge mkono Rais Samia katika zoezi hili,” amesema Shomari Kapombe Beki wa kulia wa Simba.

Naye, Clatous Chama amewaasa Watanzania kujitokeza kuhesabiwa kwani zoezi hilo hufanyika nchi zote ili kuweka utaratibu mzuri wa maendeleo ya nchi.

Chama anaungana na wachezaji wengine wa kigeni ikiwemo Joash Onyango pamoja na Victor Akpan kuwaasa watanzania kujitokeza kuhesabiwa Agosti 23, 2022.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles