Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
Jumla ya wachezaji 21 wameitwa kuunda timu ya Taifa ya watu wenye Ulemavu ‘Tembo Warriors’ kujiandaa na  mashindano ya Afrika yatakayofanyika Aprili 14-29,2024,nchini Misri
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 22, 2024, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka kwa watu wenye ulemavu Tanzania (TAFF), Athumani Lubandame, amesema tayari timu hiyo imeanza mazoezi.
” Sasa timu imeanza mazoezi rasmi ambayo yanafanyika Uwanja wa Uhuru, huku tukiwa tunasubiri maelekezo ya Serikali kuingia kambi ya pamoja baadaye,” amesema Lubandame.
Kwa upande wake, Meneja wa timu hiyo, Zaharani Mwenyemti ,amesema lengo lao ni kufika fainali ya michuano hiyo.
Amesema wanataka kwenda kutetea nafasi ya nne Afrika iliyowafanya wafuzu Kombe la Dunia ambapo waliishia hatua ya robo fainali.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salvatory Edward , ametaja majina ya wachezaji walioitwa kuwa ni Bashara Alombile, Ally Juma Abdallah, Hassan Vuai Ameri, Abdulkarim Amin Khalifa, Shadrack Hebron Sembele, Richard Fredy Swai, Ramadhan Ally Chomero.
Wengine ni Juma Mohamed Kidevu, Salimu Rashid Bakari, Steven Manumba Antony, Habibu Saidi, Salehe Mwipi, Khalfan Athumani,Emmanuel Nakala, Adamu Hassan, Lifati Anasi,Rojas Kadora, Julius Ngume, Kassimu Mohamed, Frank Ngairo na Wistin Sango.