29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunifu zaidi ya 50 kulivaa jukwaa la Swahili Fashion Week 2021

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

Wabunifu wa mavazi zaidi ya 50 wanatarajia kuuza na kuonyesha kazi zao kwa siku tatu mfululizo pamoja na kuuza bidhaa mbalimbali kwenye Tamasha la Swahili Fashion Week.

Huu ni msimu wa 14 tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo ambalo limekuwa jukwaa kubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu litafanyika Desemba 3 hadi 5, katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Swahili Fashion Week itawaleta pamoja wabunifu hao wa mavazi 50 kutoka nchi mbalimbali ili kuweza kuonyesha ubunifu wao katika kubuni mavazi ya aina tofauti kwa kutumia aina mbalimbali za malighafi.

Wabunifu watakaoonyesha mavazi katika Swahili Fashion Week kwa mwaka huu ni pamoja na Neith, Kemi Kalikawe, DD Crafts, Ninalfuca, Elsul, Bilan, Neste, Kanyali, Dapper, Jamilla Vera Swai, Ek-an-tik, Weedo, Kulwa Mkwandule, Dimass, Zuh, Chuwa, Mdc, African attirecal, Original, Angel Hudson, African Touch, Kasikana, Mshona, MK Nuru, Matana, Ashubira, Levra, Getrude SHOO, Sixfit, Bhuyeg’l, Sukaina, Ngapx, Difa, Enofits, Ucoco, Romy Jay, Noah Collection, Priscie, Scorpion,Jk Design, Jonjo, Posh By Rickie, Drax, Nyuz Cad, Clavon na Katty.   

“Pamoja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu Swahili Fashion Week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa Afrika Mashariki,”amesema Muandaaji wa Tamasha hilo, Mbunifu Mustafa Hassanali na kuongeza kuwa:

“Tunafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week, ambao watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali, Tamasha hili ambalo linazileta pamoja bidhaa mbalimbali za sanaa na utamaduni wa mswahili, pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na  maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya Kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla,” amesema Hassanali.

Kwa mujibu wa Hassanali, pamoja na maonyesho, kutakuwa na aina tofauti za ubunifu uchoraji wa hina, usukaji mikeka, ususi wa nywele sambamba na semina za aina tofauti zitakazo washirikisha wabunifu wa mavazi kabala ya kufikia siku ya shoo.

Aidha, Swahili fashion Week imeandaa tuzo zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji na weledi katika kazi za wabunifu, wanamitindo na wadau wa tania hii ya mitindo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Ili kuinua vipaji vipya vya wabunifu Swahili Fashion Week wameandaa shindano litakalo washindanisha wabuni ambao watawania tuzo ya Washington Benbella [Emerging Designers] mpaka sasa zaidi ya wabuhifu 100 wamejisajili na kushiriki shindano hilo  ambapo hivi karibuni kamati italanya mchujo wa kwanza. 

Swahili Fashion Week 2021, imeandaliwa na 361 Degrees pia wanakaribisha makampuni na tasisi mbalimbali ambao wanaweza kudhamini tamasha hilo ambalo limekuwa chachu kubwa ya maendeleo katika tasinia hii ya mitindo katika bara la Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles