30 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE WAHOJI NOTI, SARAFU KUCHAKAA

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


WABUNGE wametaka wapewe majibu na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni kwanini noti na sarafu za sasa hivi zinawahi kuchakaa tofauti na zile za zamani.

Wakizungumza jijini hapa jana katika semina iliyoandaliwa na BoT, wabunge hao walishangazwa na jinsi noti na sarafu zinavyochakaa haraka.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Ajira, Bunge, Vijana, Uratibu na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene.

Mbunge wa Viti Maalumu, Shally Raymond (CCM), alihoji ni kwanini noti za sasa zinachakaa mapema tofauti na zile za zamani hata kama zinatunzwa vizuri.

“Si kwamba hazitunzwi vizuri, hapana zinatunzwa vizuri, lakini zinawahi kuchakaa hadi unashangaa lakini zile za zamani zilikuwa zinakaa muda mrefu bila ya kuchakaa, sasa naomba majibu kwanini linatokea hili na leo (jana) nyinyi mpo hapa,” alisema Shally.

Naye, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BWL), Jaku Hashimu Ayoub (CCM), alisema kati ya mambo yanayomshangaza ni noti za Tanzania kuchakaa mapema.

Alisema wakati mwingine hata fedha zinazotolewa katika mashine za ATM’s zimekuwa zikitoka zikiwa chakavu.

“Mwenyekiti angalieni mzunguko wa fedha wa sasa noti zimechakaa, wakati mwingine hata zile ambazo tumekuwa tukitoa katika ATM’s huwa zimechakaa, ni kwanini, tunaomba majibu,” alisema Jaku.

Naye Mbunge wa Tanga Mjini, Musa Mbarouk (CUF), alihoji ni kwanini sarafu za sasa za Tanzania zimekuwa zikichakaa kwa muda mfupi.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles