30.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wabunge wa SADC wakutana Dodoma

dk-tulia-aksonNa SARAH MOSES ,DODOMA

WABUNGE wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wamekutana mjini hapa kujenga mahusiano kati yao na kujadili ugonjwa wa ukimwi.

Katika mkutano huo, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson, alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Akizungumza katika mkutano huo, Dk. Tulia aliwahimiza wajumbe hao kushirikiana kwa pamoja kujadili watakavyozishauri Serikali za nchi zao kukabiliana na maambukizi mapya ya ukimwi.

“Pamoja na kwamba kuna maambukizi mapya, dunia inapaswa kujua wanaoathirika zaidi ni wanawake na watoto.

“Hivyo basi, nawaomba wajumbe mhakikishe mnaielimisha jamii jinsi ya kupunguza unyanyapaa uliopo.

“Unyanyapaa lazima upingwe kwani unapunguza malengo ya maendeleo ya kila nchi na hivyo ni wajibu wa kila mfanyakazi kwa nafasi yake kuonyesha kujali hisia za wengine,” alisema Dk. Tulia.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kila mtu ana haki ya kupata huduma bora ya afya kwa kuwa sehemu ya mahitaji ya msingi ya binadamu.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka washiriki wa mkutano huo wa SADC, kupeleka ujumbe kwenye nchi zao juu ya uhuru wa huduma bora bila kubaguliwa.

Pamoja na hayo, alisema huduma ya uzazi salama na usawa katika jamii ni moja ya malengo yatakayoweza kuleta maendeleo ya huduma ya afya ya uzazi kwani kufikia mwaka 2030, Tanzania itakuwa imetimiza malengo hayo.

Pia, alikemea tabia ya baadhi ya wasichana kushiriki tendo la ndoa wakiwa na umri mdogo kwa kuwa tabia hiyo inaongeza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles