29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge Viti maalum CCM wahimiza Watanzania kushiriki Sensa

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Wabunge wa viti maalum wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wamewahimiza wanachama wa chama hicho kutoa shirikiano kwa makarani wa Sensa ili kufanikisha zoezi hili Agosti 23, mwaka huu.

Akizungumza katika kongamano la uhamasishaji wa sensa lililofanyika Dar es Salaam Mbunge Mwakilishi, Mariam Kisangi amesema ni muhimu kuhesabishwa kwa maendeleo ya nchi.

“Oktoba 23, kila mwananchi anatakiwa kuhesabiwa ili kupata idadi sahihi natakwmu sahihi za maendeleo,” amesema Kisangi.

Kwa upande wake Mbunge Mwakilishi wa watu wenye ulemavu, Stella Ikupa amesema ni vyema kwa watu wenye ulemavu kushiriki katika kuhesabiwa.

Alisema hata kama mtu mwenye ulemavu yupo kitandani ana wajibu wa kuhesabiwa kwa maendeleo .

“Hakuna dini inayokataza watu kuhesabiwa watu wa dini zote mnawajibu wa kuhesabiwa ili tuweze kufanikisha mpango mkakati wa maendeleo,” amesema Ikupa.

Ameongeza kuwa kwa mtu ambaye hatapata fursa ya kuhesabiwa asiridhike na hali hiyo bali afike kwa mwenyekiti wa mtaa ili aweze kupewa huduma.

“Tunajua zipo changamoto nyingi katika jamii zetu ila tusiache kutoa ushirikiano ili tuweze kuzipatia ufumbuzi pamoja na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,’ amesema Ikupa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles