25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge: Tanzania ya viwanda shakani

Leonidas  GamaNa Bakari Kimwanga, Dodoma

TANZANIA ya viwanda iko shakani kutokana na wabunge wa pande zote kushangazwa na ufinyu wa bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kuwa ndogo

Kutokana na hali hiyo, wabunge wamesema ni vigumu kuwa na Tanzania ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Akichangia hotuba ya wizara hiyo bungeni mjini Dodoma jana, Mbunge wa Songea Mjini,Leonidas  Gama alisema ya waziri mwenye dhamana ya viwanda, Charles  Mwijage kusema wakulima wa zao la muhogo wachangamkia fursa ya kulima mihogo na soko la uhakika lipo China, inakwenda

kinyume na matarajio ya Serikali.

Alisema ni vizuri Waziri Mwijage, akafuta kauli yake kuhusu soko la mihogo kuwa lipo nchini China.

“Sikubaliani kabisa na kauli ya Waziri Mwijage, kusema eti wakulima wa mihogo sasa soko  la uhakika lipo China.Je kauli hii hauoni inakwenda kinyume na sera ya Tanzania ya viwanda?, futa kauli yako, inakuaje sasa tunataka viwanda wakati mali ghafi isafirishwe nje,badala ya kila kitu kufanyika ndani.

“Ni vema ukafuta kauli yako, vinginevyo siko nawe pamoja katika hili,” alisema Gama

 

Tambwe

Kwa upande wake,Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe (CCM), alitaka maelezo ya kina ya namna mkoa huo utakavyokuwa wa viwanda, licha ya wananchi wake kuwa wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara kama tumbaku.

“Wananchi hawaelewi suala la Mkoa wa Tabora kutokuwa na viwanda,wabunge zaidi ya 12 kabla yetu walikuwa wakihoji suala hili,tunahitaji sana viwanda ili tuzalisha ajira kwa wingi hasa kwa vijana.

“Najiuliza sijui nani aliyetoa wazo la kiwanda cha tumbaku kujengwa Morogoro,waziri atuambie  nini hatima ya kiwanda cha nyuzi  pale Tabora kitajengwa.

“…Umefika wakati tupate kiwanda cha kuchakata asali,tumetenga eneo la heka 200 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na Serikali haijatozwa hata senti moja,tunachohitaji ni wawekezaji wa viwanda hivi,” alisema

 

Zitto

Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe  alitaka Bunge lisipitishe bajeti ya wizara hiyo, kwani suala la sukari halitajwa sana kama ilivyo kwa miradi ya kilimo.

Alisema katika suala la sukari kuna suala la ‘low hanging fruits’, ambapo sasa kila mwaka miwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 50,000 ya sukari huozea  katika mashamba ya Kilombero na Mtibwa.

Alisema wakulima wanalima miwa mingi kuliko uwezo wa viwanda kununua, ambapo bodi ya sukari inapaswa kutoa leseni ili vikundi vya wakulima au wawekezaji wadogo wazalishe sukari.

“Bodi ya Sukari haijatoa leseni na wala Serikali haijahamasisha Watanzania kuwekeza kwenye viwanda vidogo vya sukari ili kuwezesha miwa yote inayozalishwa kutoa sukari. Kama hili lingefanyika, leo tusingekuwa na ukali huu wa uhaba huu. Waziri wa Viwanda, hii ni ‘low hanging fruits’.

“Mheshimiwa mwenyekiti nashauri Bunge lako tukufu leo (jana), lisipitishe bajeti hii hii ikakae na Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi wawianishe mipango hii na kisha walete hapa bungeni ndiyo tupitishe. Sukari ni mfano mmoja tu katika suala hili. Hebu tumuunge mkono Rais kwa kuwarejesha mezani Wizara hizi mbili.

 

Lukuvi ajibu

 Hata baada ya kutoa hoja ya kutopitishwa kwa bajeti hiyo ambapo Zitto, aliungwa mkono na wabunge wote wa upinzani, alisimama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na kusema hoja hiyo haipaswi kuungwa mkono, bali viongozi hao walitakiwa kuwasilisha hoja yao kwa Spika wa Bunge,Job Ndugai.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonest (Chadema), alisema Serikali inafikiria kuwa na nchi inayotegemea uchumi wa viwanda,lakini haijadhamiria kufika huko.

Alisema Sh bilioni 81 zilizotengwa kwa ajili ya wizara hiyo hazitoshi.

Akizungumzia kiwanda cha Tanalek,  kinachotengeneza transofoma,  alisema Serikali inajihujumu,licha ya kuwa mwanahisa kwa asilimia 30, inanunua matransfoma kutoka India na Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles