25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi wa Habari watakiwa kufichua uvuvi haramu

Na Malima Lubasha, Serengeti

MKUU wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amewataka Waandishi wa Habari mkoani hapa kuhakikisha kuwa wanafichua vitendo vya uvuvi haramu vinavyofanyika katika Ziwa Victoria na kuonya kuwa hali hiyo inaharibu mazingira ya uhai wa ziwa ikiwemo mazalia ya samaki.

Kanali Mtambi amesema hayo jana wakati akishiriki katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari mkoani Mara yaliyofanyika mjini Musoma ambapo alizungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo ya mkoa huu badala ya kuandika mabaya.

Kanali Mtambi amesema kuwa mbali na kuwataka waandishi wa habari kufichuwa vitendo hivyo pia aliwahimiza kuandika habari za kutangaza mambo mazuri ya mkoa wa Mara, ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati inayogharimiwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema waandishi wa habari waandike habari zitakazosaidia kuhakikisha samaki wanarejea ukanda wa Ziwa Victoria ili viwanda vilivyofungwa kutokana na ukosefu wa samaki vianze uzalishaji ili kuinua uchumi wa Taifa na lishe kwa wananchi.

Amesema mkoa wa mara fursa nyingi ambazo hazijaandikwa vya kutosha kama vile Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo imekuwa ni kivutiyo kikubwa cha watalii pia uwepo wa dhahabu katika wilaya zake zote hivyo kutokana na kalamu zenu itasaidia vitendo vya uvuvi haramu kutoweka.

“Nasisitiza kuwa mnapokuwa mnatekeleza majukumu yenu ya kihabari hakikisheni mnafanyakazi kwa kuzingatia sheria na maadili ili kuepusha migogoro kati ya waandishi na jamii wakiwemo viongozi wa serikali,”amesema Kanali Mtanda.

Aidha, Kanali Mtanda alitoa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa kwa waandishi wa Habari wanapofika katika ofisi zao pale wanapozihitaji katika kutimiza majukumu yao akasema yeye kama kiongozi wa mkoa hawezi kukubali kuona mwandishi wa habari akipewa vitisho pale anapotekeleza majukumu yake.

“Waandishi wa Habari wamekuwa ni watu muhimu na msaada kwenye jamii na haitawezekana kuona watu wachache wakitoa vitisho kwa waandishi kauli hii nimeitoa kufuatia taarifa ya MRPC kwamba kuna baadhi ya viongozi haatoi ushirikiano kwa waandishiwa habari wanapofika kwao kupata ya utekelezaji wa miradi,” alisisitiza Kanali Mtambi.

Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC), Raphael Okelo amesema mkoa wa Mara una waandishi wa habari 60 na wamekuwa wakitekeleza majukumu yao licha ya kuwepo changamoto mbalimbali.

“Namshukuru Mkuu wa Mkoa na Ofisi yake kwa ushirikiano wanaota kwa waandishi wa habari wa mkoa huu na kuziomba ofisi nyingine kuiga mfano huu,” amesema Okelo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles