27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Waandishi fuateni maadili ya kazi– MCT

DSC07181NA SAFINA SARWATT, MOSHI

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kufuata maadili ya taaluma yao ili waweze kufanya kazi kwa uhuru zaidi.

Rai hiyo imetolewa jana na mwezeshaji kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT), Atilio Tagalile, alipokuwa akiwasilisha mada ya uchaguzi katika semina ya waandishi wa habari.

“Baadhi ya waandishi wa habari wamekiuka maadili ya
uandishi na wamegeuka na kuwa mashabiki wa wagombea wa nafasi mbalimbali za siasa.

“Kutokana na ushabiki huo, wameshindwa kuandika habari za kweli na zenye uhalisia ili jamii iweze kujua kinachoendelea katika siasa.

“Kwa hiyo, nawaomba ndugu zangu waandishi wa habari msikubali kurubuniwa na wanasiasa, msikubali kupotosha habari zenu, andikeni habari za ukweli ili taaluma yenu iweze kuheshimika,” alisema Tagalile.

Alisema kwamba, jukumu la wanahabari ni kuelimisha umma kuhusu hali ya nchi na mchakato mzima wa uchaguzi na siyo kuwapamba wagombea ili watakaposhinda wawape vyeo katika taasisi mbalimbali.

Naye mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Kiondo Mshana, aliwataka waandishi wa habari nchini kujenga utamaduni wa kujiendeleza kielimu ili wawe na uelewa mpana wa kuandika habari.

“Waandishi jiendelezeni kielimu, kwani uelewa mdogo wa  baadhi ya waandishi wa habari unawafanya waandike habari zisizokuwa na uhalisia na zenye uchochezi.

“Kwa hiyo, nawaomba mjitambue ili muweze kuuelimisha umma juu ya kinachoendelea nchini,” alisema Mshana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles