26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Vyombo vya habari vyashauriwa kuanzisha mijadala yenye tija

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

VYOMBO vya habari nchini vimeshauriwa kujenga tabia ya kuanzisha mijadala yenye kuchochea ukuaji wa uchumi na sio mijadala isiyo na tija kwa nchi na wananchi.

Wito huo umetolewa Oktoba 22, 2022 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, wakati akizungumzia umuhimu wa wanahabari kuchochea maendeleo, uzalishaji mali na mabadiliko ya sheria.

Sehemu ya Wahariri walioshiriki katika warsha hiyo.

Kwa mujibu wa Balile taarifa za ujenzi, uboreshaji wa viwanda, miundombinu na kilimo ambazo zitabadilisha maisha ya Watanzania kutoka katika umasikini zinapaswa kupewa nafasi zaidi kuliko zile za maisha binafsi ya watu na malumbano.

“Kwa wenzetu katika nchi zinazoendelea wanajadili namna ya kuuza biashara na viwanda vyao kwa kuzalisha bidhaa bora pamoja na kutafuta masoko, sisi hapa tuna viwanda, uzalishaji wa gesi lakini huoni mijadala mingi kwenye eneo hilo, tubadilike,” amesema Balile.

Naye, Walace Maugo, amewataka waandishi wa habari nchini kupigania haki za Watanzania na kuboresha maisha yao kupitia taaluma yao na kazi wanazozifanya kila siku.

“Kama tunavyofahamu kwamba sisi ndiyo tunaotengeneza mijadala kwenye jamii, kazi yetu kubwa ni kuhakikisha maisha bora yanapatikana na watu wanafurahia maisha katika nchi yao, tusijione wanyonge kuna hatua kubwa zimechukuliwa kutokana na kazi tunazozifanya,” amesema Maugo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles