24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vyanzo vipya vya maji vyamtesa RC Kilimanjaro

Na Safina Sarwatt, Rombo

Mgao wa maji kwa saa sita kila siku uliokuwa ukitesa wananchi zaidi ya 14,000 katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mkuu na Kijiji cha Ikuini, Wilaya ya Rombo unamuumiza kichwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.

Akizungumza juzi mkoani humo, Babu alisema hali imemlazimu kuagiza mamlaka zinazohusika kuanza tafiti mara moja kutafuta vyanzo vipya vya maji ili kumaliza kero hiyo.

“Nimeagiza Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Pangani (PBW), Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Rombo(ROMBOWSA) na Wakala wa Maji Vijijini(RUWASA) kutumia wataalam wake kufanya tafiti za kina kutafuta vyanzo vya maji na kuvifanyia usanifu ili kukabiliana na upungufu huo.

“Hata, kwa sasa juhudi zinafanyika kutafuta vyanzo vya maji katika maeneo ya Kilema, Kibosho ili miradi mingine mikubwa itakapopatikana iweze kunufaisha vijiji vilivyopo ukanda wa juu na kujengwa kwa wakati muafaka,” amesema Babu.

Mkuu huyo wa mkoa pia ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji awamu ya kwanza, ambao ni ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa kuchukua lita za ujazo 500,000, mradi unaotekelezwa na ROMBOWSA, kwa gharama ya zaidi ya Sh milioni 192.

Aidha, Babu amesema:”Hawa wataalamu wafanye hiyo kazi haraka iwezekanavyo, hatutaki malalamiko ya wananchi kuhusu maji maana fedha zipo, Mheshimiwa Rais ana fedha na sitaki kuona tunakwamishwa kwa namna yoyote ile.

“Namshukuru Rais kwa kutoa fedha nyingi za maji mkoa wa Kilimanjaro, namshukuru Mbunge wa Rombo, Profesa Adolf Mkenda kwa kuhakikisha kero ya maji kwa wananchi wake zinapatiwa ufumbuzi,” amesema Babu.

Babu alienda mbali zaidi akisema miradi ya maji ambayo inatekelezwa wilayani humo yenye jumla ya zaidi ya Sh bilioni 7.6 bilioni itazalisha maji kiasi cha lita za ujazo milioni 6.9 kwa siku ambalo ni sawa na ongezeko wastani wa asilimia 77.

“Najua Rombo kuna tatizo kubwa sana la maji lakini kwa mkakati huu na mambo tunayoyafanya, serikali hii ya awamu ya Sita ya mama Samia Suluhu Hassan, Rombo itakuwa historia ya kupata maji, mtapata maji ya kutosha hapa Rombo,” amesema Babu.

Katika hatua nyingine, Babu amesema katika bajeti ya mwaka 2023/24 Mamlaka ya maji Rombo ina mpango wa kuchimba visima 17 vya maji kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa maji katika vijiji vya ukanda wa chini hasa wakati wa kiangazi ambapo wanawake wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta maji.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Rombo(ROMBOWASA), Martin Kinabo, amesema katika wilaya hiyo kunatekelezwa miradi mbalimbali ya maji ikiwemo miradi 6 ambayo itagharimu zaidi ya Sh bilioni 8 ambayo inaendelea na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

“Mradi wa uboreshaji wa huduma katika mji wa Mkuu na kijiji cha Ikuini ni moja wapo ya miradi 6 inayotekelezwa katika wilaya ya Rombo, mradi huu unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo sehemu ya kwanza imetekelezwa kwa mfumo wa “force Account” na Rombowssa,”amesema Kinabo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles