24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Vyama vyatakiwa kufanya kampeni za kistaarabu Hai

Na Safina Sarwatt-Hai 

VYAMA vya siasa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro vimetakiwa kufanya kampeni za kistaarabu na kufuata taratibu na kanuni za nchi.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Hai, Lwelwe Mpina jana wakati akipokea msaada ya mifuko ya saruji 100 iliyotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa  Kilimanjaro kwa ujenzi wa mradi wa nyumba za Jeshi la Polisi.

Mpina alisema kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wanasiasa wanatakiwa kufanya kampeni za kistaarabu bila kutumia lugha chafu zenye kuleta viashiria vya uvunjivu wa amani na vurugu. 

“Nawahisi ndugu zangu wanasiasa kipindi hiki, hakikisheni mnalinda amani ya nchi, acheni kutumia lugha chafu, uzeni sera za vyama vyenu, acheni kutumia lugha za matusi muheshimu kanuni na sheria za nchi,” alisema Mpina. 

Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kuimarisha hali ya ulinzi na usalama kwa vyama vyote vya siasa wakati wa mikutano ya kampeni. 

“Tumejipanga vema kuhakikisha tunaimarisha ulinzi na usalama kwa vyama vyote vya siasa bila ubaguzi, na uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu,” alisema Mpina. 

Alisema askari wake wamejipanga kusimamia kampeni kwa uaminifu na uadilifu ila anatoa angalizo kwa vijana wanaotumika vibaya na kuleta vurugu  hatasita kuwachukulia hatua za kisheria. 

Meneja wa NHC, Juma Kiaramba alisema msaada huo ni sehemu ya mapato ya ukusanyaji kodi kwa wapangaji wa shirika hilo, na kwamba mwaka huu wamefanikiwa kukusanya Sh bilioni 2.8 sawa na asilimia 98 ya malengo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles