24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Vyakula vya kwenye sherehe, misiba kupimwa


RENATHA KIPAKA, BUKOBA

KAMATI ya Lishe ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imemtaka Ofisa Afya wa wilaya hiyo, Clara Macha kuwaandikia barua watendaji wake ngazi za kata na vijiji kupima vyakula katika sherehe na mikusanyiko mingine kabla ya kuliwa.

Vilevile imemtaka Clara kuhakikisha wanafunzi wa bweni wanakula chakula kilichowekewa chumvi yenye madini joto.

Maazimio hayo yalifikiwa katika kikao cha mapitio ya mpango wa lishe kilichofanyika katika Halmashauri ya Bukoba Vijijini jana.

Kamati hiyo ilisema   barua hiyo ipite  ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Bukoba  watendaji hao waweze kutekeleza agizo hilo.

Kuhusu madini joto, kamati ya lishe ilisema kuna shule mkoani humo ambazo zimekuwa zikitumia chumvi  iliyochimbwa na kuhifadhiwa kienyeji.

“Mbali na chunvi, shule hizo za kulala ziwe na bustani  wanafunzi wawe wanapata mlo kamili wenye mbogamboga na matunda,”ilisema kamati hiyo.

  Ofisa wa maabara wa halmashauri hiyo, Sagamambi Mjinja alisema maofisa afya wamekuwa wakitekeleza agizo hilo hivyo hatua hiyo inawakumbusha kuwajibika zaidi.

“Suala la kupima vyakula katika sherehe au mikusanyiko ni jukumu lao ambalo wamekuwa wakilitekeleza kila siku, hivyo barua hiyo ni ya kuwaongezea umakini  kuhakikisha wanatekeleza kwa ufasaha jukumu hilo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles