29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Vodacom na Infinix wazindua simu mpya ya Infinix NOTE 8

Mwandishi wetu

Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kidijitali nchini, Vodacom Tanzania PLC, kwa kushirikiana na Infinix leo imetambulisha rasmi simu mpya aina  ya Infinix NOTE 8. itaambatana na ofa ya GB 96 za internet kutoka Vodacom Tanzania PLC kwa Mwaka mzima.

Vodacom Tanzania PLC wanashirikiana kuifikisha Infinix NOTE 8 kwa Watanzania ili kuhakikisha kila mtanzania anaingia katika ulimwengu wa kidijitali kwa kumiliki simu bora na kupitia mtandao wenye kasi ili kufurahia maendeleo ya teknolojia duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi, Afisa wa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa alisema, NOTE 8 ina  uwezo wa kuhimili application zenye ujazo mkubwa pasipo simu kupata moto au kuzimika ghafla wakati wa matumizi. 

“Pamoja kuwa na processor kubwa yenye kukufaidisha wewe mpenzi wa games, kazi nyingi za kiofisi na za shuleni lakini pia Infinix NOTE 8 ina sifa nyingine pendwa kama vile, kamera mbili za mbele zenye MP 16 na kamera 6 nyuma zenye MP 64, chaji yenye kujaza battery ya ujazo wa 5200mAh, kioo cha inch 6.95 na memory ya GB 128Rom kwa GB 6Ram”.alisema Karupa

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella, alisema kwamba nia ya kampuni ya Vodacom ni kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, ili kulitimiza hili hawana budi kuhakikisha wateja wanapata huduma za Intaneti bila kikwazo chochote.

“Umuhimu wa mtandao wenye kasi kwa kila mtumiaji wa smartphone unajulikana, na ili watanzania tusiwe nyuma ya ukuaji wa teknolojia tunahitaji mtandao wenye kasi ili kujifunza mambo mapya kila leo na kwa kulizingatia hilo Vodacom Tanzania PLC inakusogeza karibu na ulimwengu wa kidijital kupitia ofa ya GB 96 katika kila simu ya Infinix NOTE 8 kwa muda wa mwaka mzima,” alisema Nandi. 

Infinix na Vodacom Tanzania Plc wamekuwa washirika kwa muda mrefu tangu kuzinduliwa rasmi kwa bidhaa za Infinix nchini.  

Kampuni hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kuleta mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini, simu hii ya Infinix Note 8 inapatikana katika maduka yote ya Vodacom naya Infinix yaliyopo maeneo yote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles