25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Viti Maalumu waingia kazini Kagera

Na NYEMO MALECELA-KAGERA

WAGOMBEA ubunge Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera wamewaomba wapigakura kuwachagua wagombea wa chama hicho majimbo yote mkoani humo, ili waweze kuwaletea maendeleo zaidi.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM Mkoa wa Kagera, mgombea ubunge Viti Maalumu, Benadeta Mshashu alisema Serikali inayoongozwa na CCM imejenga hospitali tatu za wilaya, vituo vya afya zaidi ya 14, ambapo kuna wodi za watoto, mama wajawazito na vyumba vya upasuaji ambavyo vimesaidia kupunguza vifo vya kina mama wakati wanajifungua.

“Kwa upande wa vijana imewajengea chuo kikubwa cha Veta, shule kongwe za Rugambwa, Nyakato, Kahororo na Ihungo zote zimekarabatiwa zimekuwa mpya.

 â€œMeli mmeiona? Wafanyabiashara, biashara imeanza kuchangamka hata ndizi zilizokuwa zimepungua bei kutokana na kukosa soko zimeanza kupanda bei kutokana na kurahisishwa kwa usafirishaji wake kwenda mikoa jirani, hasa Mwanza ambako kuna soko kubwa kwa kutumia usafiri wa meli,” alisema Benadeta.

Mbunge Mteule kupitia Viti Maalumu Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Regina Zachwa alisema wabunge wanawake wamekuwa msaada mkubwa katika kuifikia jamii, hivyo wananchi wa Mkoa wa Kagera wanaombwa kuwachagua wabunge wa CCM wa majimbo yote na kuwawezesha wabunge wanawake watatu wa mkoa huo kuingia bungeni. 

“Wanawake ndio jamii yenyewe kwa sababu mwanamke ni mlezi wa familia ambayo inahusisha baba, watoto na rasilimali zote za kifamilia.

 â€œWabunge wa kike tunafanya kazi sawa na wabunge wa wanaume, kazi tunazopewa ni zile zile ndio maana wakateuliwa wabunge Viti Maalumu ili waweze kuifikia jamii kiurahisi,” alisema Regina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles