32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Afrika wakutana kujadili corona

Addis – Ababa, Ethiopia

VIONGOZI kadhaa wa nchi za Afrika, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom, na Rais wa Ufaransa wamekutana na kujadili njia za kukabiliana na ugonjwa wa corona au Covid-19 barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa, mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video kwa lengo la kuchunguza njia ambazo nchi za Afrika zinaweza kutumia katika kukabiliana na janga la corona na pia ushirikiano na jamii ya kimataifa kuhusiana na janga hilo, umehudhuriwa na Mkurugenzi wa WHO, Rais wa Afrika Kusini na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika (AU) Cyril Ramaphosa. 

Wengine waliohudhuria ni marais  Uhuru Kenyatta wa Kenya, Ibrahim Boubacar Keita wa Mali, Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Abdel Fattah el-Sisi wa Misri, Macky Sall wa Senegal, Paul Kagame wa Rwanda na Emmerson Mnangagwa wa Ethiopia.

Aidha Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa walihudhuria kikao hicho pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki.

Hali kadhalika Mkurugenzi wa Vituo vya Umoja wa Afrika  vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa John Nkengasong alihudhuria kikao hicho.

Washiriki walisisitiza ulazima wa kuimarisha uwezo wa maabara za kupima corona na kuanzisha mfumo salama wa uchukuzi na usafiri barani humo. 

Kukosekana uwezo wa kutosha katika sekta ya afya katika aghalabu ya nchi za Afrika kumepelekea kuibuka wasi wasi kuhusu kuenea virusi vya corona barani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles