25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Wanajeshi wa Rwanda watuhumiwa kubaka

Kigali, Rwanda

ASKARI watano wa Rwanda wamekamatwa baada ya wakazi wa kitongoji kimoja cha Mji Mkuu Kigali kudai waliwabaka wanawake walipokuwa wakitekeleza sheria ya kukaa nyumbani iliyowekwa kote nchini humo ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jeshi la Rwanda limethibitisha habari hiyo ya kutiwa mbaroni wanajeshi hao. Wakazi wa kitongoji cha Nyarutarama waliiambia ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa jeshi pia kwamba askari waliwapiga wakazi na kuwaibia mali zao.

Mmoja wa waathirika aliwambia waandishi wa habari kuwa, mnamo Machi 26, mwanajeshi aliyekuwa amejihami kwa silaha aliingia kwa nguvu katika nyumba yake na kumpiga mume wake, alipokuwa akijaribu kuingilia kati kumzuia askari asimbake.

Serikali ya Rwanda iliweka sheria ya kutotoka nje kote nchini humo ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, lakini baadhi ya wakazi wamekuwa wakilalamika juu ya ukatili wanaofanyiwa na maofisa wa usalama wanaosimamia utekelezwaji wa sheria hiyo.

Wiki iliyopita wanaume wawili walipigwa risasi na kuuawa walipopatwa wakitembea nje. 

Polisi ilisema kuwa wanaume hao walijaribu kuwashambulia maofisa wa polisi. Matukio ya upigaji na hata mauaji dhidi ya raia yanayofanywa na vikosi vya usalama yameshuhudiwa pia katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Nchini Kenya na Uganda watu kadhaa wameshauawa hadi sasa kufuatia vitendo vya utumiaji mabavu vinavyofanywa na polisi wakati huu wa utekelezwaji wa sheria ya kutotoka nje usiku.

Hadi sasa Rwanda imethibitisha visa 89 vya maambukizo ya virusi vya corona huku Marekani ikiendelea kushikilia rekodi ya kuwa na wagonjwa wengi zaidi wa Covid-19 ambapo hadi sasa karibu watu 280,000 wameambukizwa virusi hivyo katika nchi hiyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles