30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana watakiwa kutumia fursa za elimu kujiajiri

Na Raymond Minja, Mafinga

Vijana kote nchini wametakiwa kujituma na kujitafutia fursa mbalimbali za ajira kupitia mafunzo ili kuweza kujiajiri na kujingizia kipato kitakachowasadia kuendesha maisha yao kuliko kukaa vijiweni na kuanza kusubiri ajira kutoka serekalini pindi wanapomaliza masomo yao .

Rai hiyo imetolewa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi, James Mgego wakati wa ufunguaji mafunzo ya kilimo biashara kwa vijana zaidi ya mia saba 700 katika zao la parachichi yaliyoandaliwa na taasisi ya (MUYOWIRUDE(iliyoko wilayani Mufindi mkoani iringa yenye lengo la kumkwamua kijana kwenye umaskini kwa kuwapa elimu ya ujasiriliamali ili waweze kujiajiri wenyewe.

Mgego alisema kuwa kwa sasa swala ajira ni changamoto kwani wanaomaliza elimu za juu ni wengi hivyo ni ngumu kwa serekali yoyote duniani kuweza kuwajiri watu wake wote hivyo ni vema vijana kutumia fursa na elimu za ujasiriliamali wanazopata ili kwenda kujiajiri na hata kuajiri wengine .

Alisema serekali kupitia taasisi zake na mashirika ya watu binafsi imekuwa ikishirikiana nao ili kutoa mafunzo ya ujasiriliamali kwa vijana mbalimbali ili waweze kujiajiri na kuajiri wengini

“Nichukue fursa hii kuipongeza taasisi hii ya (MUYOWIRUDE) kwa kuamua kujitoa kwa moyo wa uzalendo kutoa mafunzo kwa vijana wetu hawa, na niwapongeze vijana mmekuja kwa wingi basi nanyi mjitoee kupokea maarifa haya ili muweze kwenda kutumia elimu muliopata leo kujiajiri huko muendako,” amesem.
.
Alisema kuwa ili mtuu yeyote aweze kufanikiwa katika jambo lolote hakuna budi kujitoa kwa hali na mali ili kuweza kutimiza ndot zake hivyo wao kama chama wataendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuweza kufanikisha jambo lolote linalohusu kufungua fursa kwa vijna kujiajiri .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Marco Shayo alisema taasisi hiyo iliyoanzishwa na vijana wazalendo waliomaliza elimu ya Chuo Kikuu ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa vijana na kinamama ili kuwaondoa njaa na umaskini kwa kuwapa elimu ya ujasiriliamali .

Alisema kuwa kwa sasa taasisi hiyo imeamua kutoa mafunzo kwa vijana kwenye elimu ya kilimo biashara cha zao la parachichi kwani zao la hilo limekuwa ni zao la kibiashara ambalo soko lake ni kubwa hapa nchi.

Alisema kwa sasa wanatoa elimu hiyo kupitia tasisi ya mamlaka ya elimu Tanzania kupitia mradi wa( SDF ) kwa vijana wenye sifa kuanzia miaka 15 hadi 35 ikiwa na lengo lile lile la kumuongezea maarifa kijana ili kuweza kupata elimu na kujiajiri na kuajiri wengine.

Alisema mara baada ya wanafunzi hao kupata elimu watakwenda kufanyakazi kwa vitendo ili kwenda kujifunza kwa vitendo kwa uzalishaji wa parachichi, upandaji wa parachichi, kutengeneza vifungashio na wengine kwenda kutengeneza maboksi kwa ya kuhifadhi parachichi.

Hata hivyo alisema kuwa wahitimu wote watapewa fedha za feld na serekali ili kuweza kujikimu wakati wanafanya mafunzo mbalimbali huko watakaopangiwa kwenda kushiriki mafunzo hayo kwa vitendo .

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Jakson Michael alisema kuwa elimu aliyoipata kupitia mafunzo hayo imempa mwanga na njia ya mafanikio kwani atakwenda kutumia elimu hiyo kujiajiri kwa kulima kilimo biashara cha barachichi ili kuja kuwa milionea wa baadaye .

Michael alisema kuwac kabla ya kupata elimu hiyo alikuwa hana lengo la kulima zao la biashara la parachichi kwani aliona kuwa litampotezea muda mrefu lakini mara baada ya kupata elimu hiyo ameona kuwa alikuwa amechelewa sana kuanza kilimo hicho kwani angekuwa ameanza toka awali basi ungekuta amefika mbali.

Naye, Rashidi Lulimbo kutoka kata ya mdabula alisema elimu hiyo imekuja muda muafaka kwani tayari yeye alishaanza kuotesha miche ya parachichi zaidi ya 1,000 na kupanda miche zaidi ya 300, hivyo kupitia maarifa aliyopata anaamini kilimo chake cha parachichi kitakwenda kuwa bora zaidi kuliko apo awali .

Rashidi aliwataka vijana kute nchini kuweza kutumia vema fursa za mafunzo ya ujasiriliamali pindi zinapotoke kwani ni adimu sana kupata fursa za mafunzo ya ujasiriliamali bure kama wao walivyoweza kupata elimu hiyo bure kupitia (MOYOWIRUDE).

Katika mafunzo hayo wanafunzi hao waliweza kupewa elimu juu ya aina ya miche na faida zake, jinsi ya upandaji wa miche na umbali wa upandaji, elimuu juu ya kuchanganya udongo na mbolea wakati wa upanda na jinsi ya kutibu magonjwa mbalimbali yanayoshambulia mmea wa parachichi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles