27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana washauriwa kuwa watetezi wa haki

Asha Bani, Dar es Salaam

Vijana zaidi 100 nchini wamekutana kwa ajili ya kujengewa uwezo wa kuwa watetezi wa haki za binadamu.

Vijana hao ambao ni wanafunzi na wengine kutoka klabu za haki za binadamu walielezwa umuhimu wa kuwa watetezi katika maeneo wanayotoka kwa ajili ya kutetea jamii.

Akizungumza wakati wa kufungua kongamano la vijana katika kuadhimisha miaka 70 ya watetezi wa haki za binadamu, Mratibu Mshauri wa nchi za Jumuiya ya Umoja Ulaya nchini Tanzania, Helge Flarg, amesema kuwa mtetezi wa haki za binadamu si lazima kuwana taaluma au umesomea ni wakati na mahala popote unakuwa na uwezo wa kutetea haki za wananchi.

“Sio lazima kuwa na elimu katika kutetea wananchi katika kulinda amani na kutetea haki za wanyonge bali kila kijana ana uwezo wa kufanya hivyo kwa ajili ya kulindana kutetea haki za binadamu,” Flarg.

Naye Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa amewataka vijana waliokuwa mashuleni na vyuoni kuanza kuwa watetezi wa haki za binadamu ili kuweza pia kutetea haki zao..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles