26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Vigogo waangukia pua Wazazi CCM

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

VIGOGO wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwamo, Dk. Edmund Mndolwa na Paul Kirigini wameangukia pua katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho uliofanyika juzi katika Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

Ikumbukwe kuwa Dk. Mndolwa alikuwa akitetea nafasi yake ya Uenyekiti huku Kirigini alikuwa akisaka uwakilishi wa Jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.

Katika nafasi ya Mwenyekiti, jumla ya kura zote zilizopigwa zilikuwa 837, ambapo idadi ya kura halali ilikuwa 835 na zilizoharibika zilikuwa mbili.

Hivyo, katika matiokeo hayo, Fadhili Mganya alipata kura 574 akifuatiwa na Dk. Edmund Mndolwa aliyepata kura 64 na Mwanamanga Mwaduga aliyepata kura 61.

Wengine ni Ally Othman aliyepata kura 57, Said Mohamed kura 43, Bakari Kalembo kura 21, Zahara Haji kura 6 na Ally Masoud kura 5.

Katika nafasi tatu za UNEC Tanzania Bara Wagombea wa nafasi hiyo ya Nec Bara kupitia Jumuiya ya Wazazi, walikuwa 14.

Hamoud Jumaa alipata kura 561 akifuatiwa na Doto Biteko(Waziri wa Madini) kura 535, George Gandye kura 238.

Waliobwagwa katika uchaguzi huo ni Dk. Angelina Mabula(Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) aliyepata kura 232 akifuatiwa na Paul Kirigini aliyepata kura 215.

Mbali na Kirigini wengine walioangukia pua ni Adam Malima(Mkuu wa Mkoa wa Mwanza) aliyepata kura 195, Kelvin Tegwa kura 176, Angela Kiziga aliyepata kura 113.

Pia kuna Mgore Kigere aliyepata kura 58, Mohamed Ngingite kura 46, Sayi Daniel kura 41, Mecktridis Mdaku kura 27, Bupe Mwakang’ata kura 26 na Nyiriza Nyiriza aliyepata kura 21.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles