22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

VIGOGO TASAF WATUMBULIWA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki.

Na LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, amewasimamisha kazi vigogo watano wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) kwa kushindwa kusimamia vema mfuko huo na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni sita

Vilevile ameagiza kusimamishwa kazi maofisa washauri na ufuatiliaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu wapatao 106 wa halmashauri mbalimbali nchini.

Maofisa hao wanadaiwa kushindwa kufuatilia na kusimamia mpango huo na kusababisha kaya zisizostahili kuingizwa kwa mpango na kulipwa kinyume na utaratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri Kairuki alisema  kuanzia Januari 2014 hadi Septemba 2016  Sh  6,427,110,309 zimeokolewa baada ya kaya 42,035 zisizo na sifa za kuingizwa katika mpango huo.

Alisema amewasiliana na waziri wa TAMISEMI na tayari ameshaelekeza waratibu wa TASAF wilaya wasimamishwe kazi na uchunguzi wa jinsi walivyojihusisha kuvuruga utekelezaji wa mpango huo hadi kufikia kuandikisha kaya zisizo na sifa, ufanyike.

“Naagiza ufanyike uchunguzi wa kina kubaini ushiriki wa maofisa hao na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaothibitika kuhusika katika kuvuruga utaratibu wa utekelezaji wa mpango au kuwapo udhaifu katika usimamizi ufuatiliaji na uwajibikaji.

Alimtaka Mkurugenzi wa TASAF kuhakikisha uchunguzi huo unakamilika katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja kuanzia jana.

Alisema baada ya kufanyika mchanganuo  ilibainika kaya 13,898 zilikuwa na mwanakaya mmoja au wote wamefariki dunia, 6228 walihama mitaa au vijiji ambako mpango haujaanza kutekelezwa, 17,746 hawakujitokeza hata mara moja kupokea ruzuku.

Kaya 13,468 zilithibitishwa kuwa siyo maskini huku kaya 4,352 zilibainika kuwa na wanakaya ambao ni wajumbe wa kamati za usimamizi za jamii, halmashauri za vijiji, kamati za mitaa, viongozi na watendaji.

Alisema baada ya Februari kuziagiza halmashauri zote nchini kufanya uhakiki kubaini kaya zisizo na sifa kuandikishwa katika mpango huo, ilibainika  kaya zipatazo 55,692 hazikuwa na sifa ya kunufaika na mpango huo.

“Kaya 55,692 zimeondolewa kwenye mpango kutokana na sababu mbalimbali.

“Sababu hizo ni pamoja na vifo, iwapo kaya ni ya mtu mmoja au wanakaya wote kufariki dunia.

“Sababu nyingine ni kaya kuhamia kijiji au mtaa ambako haujaanza kutekelezwa na kutojitokeza mara tatu mfululizo kupokea ruzuku,” alisema Kairuki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles