27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

VIGOGO CCM, UKAWA KUTIKISA KAMPENI

Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Emanuel Kawishe
Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Emanuel Kawishe

PATRICIA KIMELEMETA, DAR ES SALAAM

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iko mbioni kutoa mwongozo wa viongozi wa kitaifa kuhudhuria kampeni za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Januari 22, mwakani.

Kazi hiyo itafanyika baada ya kukamilika kwa uteuzi wa majina ya wagombea katika nafasi mbalimbali.

Tayari NEC imetoa ratiba ya uchaguzi huo utakaofanyika katika kata 22 nchini na Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar, ambapo mbunge wake Hafidh Ally Tahir (CCM) alifariki dunia Novemba 11 mwaka huu mjini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Emanuel Kawishe, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, tume imetoa mwongozo wa maadili na taratibu zitakazotumika katika kampeni.

“Hatuwezi kusema sasa hivi kuhusiana na viongozi wa kitaifa kwa sababu muda bado, ukifika tutatoa mwongozo,” alisema Kawishe.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Desemba 10 hadi 22, mwaka huu Tume itatoa fomu za uteuzi kwa wagombea waliopitishwa na vyama vya siasa na Desemba 22 ni uteuzi wa wagombea.

Kampeni za uchaguzi zitaanza kutimua vumbi Desemba 23 hadi Januari 21, mwakani na Januari 22 ni siku ya kupiga kura.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, alisema uchaguzi huo mdogo Amesema kuwa, vyama vya siasa vinapaswa kuandaa wagombea wao.

“Nafasi hizo zinajazwa kwa mujibu wa vifungu vya 37(1)(b) na 46(2) vya sheria ya taifa ya uchaguzi, sura ya 343 na vifungu vya 13(3) na 48(2) vya sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa sura ya 292.

“Ratiba ya uchaguzi iliyotolewa itasaidia wananchi kupata uwakilishi wa nafasi hizo baada ya kujitokeza kwa mambo mbalimbali yaliyosababisha wawakilishi wao kutokuwepo.

“Tumetoa ratiba ya uchaguzi mdogo kwenye kata 22 na jimbo moja la Dimani baada ya wananchi wa maeneo hayo kukosa uwakilishi kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mbunge wa Dimani kufariki hivi karibuni,” alisema.

Jaji Lubuva alisema vyama vy siasa vinapaswa kuzingatia ratiba iliyotolewa ili kuondoa malalamiko yasiyo na msingi.

Mikoa ambayo kata zake kwenye mabano zitafanya uchaguzi ni pamoja na Dar es Salaam (Kijichi),Dodoma (Ng’hambi) na (Ihumwa), Morogoro(Kiwanja cha Ndege),Iringa(Igombavanu),Arusha(Ngarenanyuki) na (Mateves).

Mingine ni pamoja na Singida (Kinampundu), Shinyanga (Isagehe), Katavi (Kasansa), Mwanza (Malya) na (Kahumulo), Ruvuma (Maguu) na (Tanga), Kagera (Kamwani), Geita (Nkome), Kilimanjaro (Lembeni), Mara (Mkoma), Manyara (Duru), Simiyu (Mwamtani) na Pwani (Misugusugu).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles