Susan Uhinga, Tanga
Baraza laUmoja wa Wanawake Wilaya ya Tanga (UWT) limetoa tamko la kumpongeza mwenyekiti wao wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Dk. John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Watanzania.
Akisoma tamko hilo leo Jumapili Desemba 16, mwenyekiti wa UWT wilaya ya Tanga Moza Shillingy amesema kazi zinazofanywa na Rais Magufuli ni kubwa na za kuonekana wazi hivyo juhudi hizo zinapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote wapenda maendeleo.
Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake mambo makubwa yamefanyika yakiwamo ujenzi wa reli ya kisasa itakayotumia treni ya umeme , ameboresha huduma ya afya kwa kupanua vituo vya afya nchi nzima , elimu bila malipo , ametekeleza kwa vitendo kampeni yake ya kumtua mama ndoo kichwani kwa, kusimamia nidhamu kwa watumishi.
“Mambo mengine ni kutoa kipaumbele kwa wanawake katika nafasi za uongozi , mradi mkubwa wa bomba la mafuta , upanuzi wa bandari ya Tanga utaopelekea kutia nanga kwa meli kubwa pamoja na kusimamia haki za wanyonge, “ amesema Moza.
Aidha baraza hilo limetoa rai kwa wanawake wote nchini katika kuumunga mkono Rais Magufuli wahakikishe wanawandaa vijana katika maadili mazuri hasa uzalendo ili waweze kufaidika katika fursa za miradi mikubwa ya serikali.