24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

UVCCM YAVUNJA UKIMYA KWA LOWASSA, MBOWE

Na Mwandishi Wetu-Dar es Salaam


UMOJA wa Vijana  wa CCM  (UVCCM),  umewataka Watanzania kuyapuuza madai ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ya kumtaka Rais Dk.  John Magufuli aruhusu mjadala wa Katiba Mpya ili kuachana na vita ya uchumi, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Hayo yalisemwa juzi na Kaimu Katibu  Mkuu wa UVCCM,  Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza kuhusu kauli ya Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, wakati wa kampeni za udiwani mkoani Arusha pamoja na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuhusu suala la Katiba Mpya ya nchi.

Shaka  alisema kinachotamkwa na Lowassa ni mkakati  wa majaribu hatari ili kuitia nchi kwenye machafuko, ghasia na fujo kwa nia ya kuitoa  Serikali kwenye mwelekeo wa  utekelezaji wa Ilani  ya  Uchaguzi  ya CCM ya  Mwaka 2015/2020 .

“Tunawapa  tahadhari  wananchi wasikubali  kufuata mkumbo wa siasa za kibabe za Lowassa na Chadema kudai katiba  mpya kibabe. Katiba  iliyopo ni ya kidemokrasia imeliongoza Taifa  kwa miaka  54 ya Uhuru na Muungano,” alisema Shaka

Alisema uzuri wa Katiba iliyopo unafahamika na lowasa pamoja na Chadema kwani hata Lowassa ikiwa mbunge wa Mondoli kwenye Bunge Maalumu la Katiba, alipiga kura ya ndiyo kupinga Mapendekezo ya Rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba na kukataa Muungano wa serikali tatu..

Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema matatizo ya wananchi ni kupata huduma  za afya, maji safi na salama, elimu yenye ubora,ujenzi wa barabara za lami na ajira wala si katiba kwani katiba iliopo inakidhi haja.

“UVCCM tunajua Afrika inajua na dunia inafahamu kasi ya Rais na utendaji wa Serikali yake si ya kawaida katika kuwatumikia  wananchi. Jaribio lolote la uharibifu wa amani lazima likabiliwe kwa nguvu zote,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles