26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

UVCCM WATWANGANA NGUMI ARUSHA

Wapambe wa wagombea wa wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), leo wametwangana hadharani wakituhumiana kuwa matapeli wa kisiasa.

Vurugu hizo zilijitokeza leo Ijumaa, Septemba 22 kabla ya uchaguzi wa nafasi hizo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, vurugu hizo zinadaiwa kudumu kwa dakika zisizozidi 20, zilitokana na wapambe wa wagombea Jimmy Pamba na Godliving Kisila kutofautiana kauli.

Mmoja wa wapambe wa Kisila, Hussein Abdallah anadaiwa kumtuhumu Lameck Dudu ambaye anadaiwa kuwa kambi ya Pamba kuwa si mjumbe wa mkutano huo na ni tapeli wa kisiasa hivyo hakupaswa kuwepo katika uchaguzi huo.

Baada ya kauli hiyo Dudu anadaiwa kumrushia ngumi na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Sylvester Meda na kuanguka chini, hali iliyosababisha wapambe wengine wa pande zote mbili kutokukubaliana na hali hiyo na kuanza kupigana.

“Wamenipiga na kunichania nguo zangu lakini sijui kosa langu ni lipi, UVCCM Arusha imezungukwa na wahuni, chama kinapaswa kuwachukulia hatua wote walioiabisha Jumuiya kwa maslahi yao,” amesema Meda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles