25.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Utafiti: Watu milioni 10 watakufa kwa saratani mwaka huu

HASSAN DAUDI Na MITANDAO

SARATANI ni miongoni mwa magonjwa yanayoitikisa dunia kwa sasa kutokana na kusababisha vifo vya watu wengi duniani.

Wataalamu wa masuala ya afya wanasema si tu binadamu anayeweza kupata ugonjwa huu, bali viumbe hai vyote, wakiwamo wanyama wa porini kama simba, chui na wengineo.

Licha ya juhudi zinazofanywa na serikali za mataifa mbalimbali ikiwamo uwekezaji mkubwa wa fedha katika kukabiliana nao, imeonekana kuwa bado vita dhidi ya saratani inahitaji nguvu zaidi.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Tafiti za Saratani (IARC), umegundua kwa mwaka huu pekee, wagonjwa wapya wamefikia milioni 18.1 huku vifo vikiwa ni milioni 9.6.

Kuthibitisha kuwa saratani imeongeza kasi ya kuhatarisha uhai wa binadamu, miaka sita iliyopita wagonjwa walikuwa ni milioni 14.1 na vifo vilitajwa kuwa ni milioni 8.2.
Utafiti huo pia umebaini kuwa ugonjwa huo unaweza kuua watu milioni 10 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Taarifa yake inaongeza kuwa mmoja kati ya wanaume watano atakuwa na saratani na kwa upande wa wanawake, ni mmoja kati ya sita, huku hali hiyo ya hatari ikitarajiwa kuwa hivyo kwa kipindi chote cha karne ya 21 kilichobakia.

Mkurugenzi wa IARC, Christopher Wild, anasema utafiti huo umeonesha ni kwa kiasi gani mapambano dhidi ya saratani yalivyo na safari ndefu.

“Hiyo inaonesha ni kwa kiasi gani kazi kubwa imebaki katika kuondosha mzigo mkubwa wa saratani duniani kote. Bado kuna kazi katika kukabiliana nao,” anasema Wild.

Mtaalamu huyo anashahuri kuwa vita hiyo inatakiwa kwenda sambamba na kampeni za kuhamasisha watu kufanya mazoezi, kuacha uvutaji sigara na kula vyakula kwa mpangilio (balanced diet).

Mtaalamu wa afya kutoka Mexico, Vanessa Fuchs, naye anaunga mkono suala hilo akisema umakini wa hali ya juu unapaswa kuchukuliwa.

“Kukosekana kwa mpangilio wa vyakuala kuna uhusiano mkubwa na saratani ya matiti. Chai ya kijani inaweza kuzuia seli za saratani,” anasema Fuchs ambaye hoja yake inaendana na utafiti uliowahi kufanywa na Jarida la Afya la PLOS Medicine.

Fuchs anawashauri watu kuacha utamaduni wa kula nyama za kusindika.
Pia anaonya juu ya matumizi ya chumvi nyingi na vyakula vyenye sukari nyingi, akisema hali hiyo inaweza kumsababishia mlaji kupata saratani.

Anawataka watu kuwa na mazoea ya kula matunda na mboga mboga, akiusisitiza utamaduni wa kutokosa maharagwe, njegere au kunde katika milo yao ya kila siku.
“Kufanya hivyo kutaepusha kwa kiasi kikubwa kasi ya vifo vinavyotokana nasaratani ya tumbo, maini, ulimi, mapafu na matiti,” anasema.

Sguruka la Afya Duniani (WHO) lilitoa takwimu kuhusu vifo vinavyotokana na saratani ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, jumla ya watu milioni 8.8 walipoteza maisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles