30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Urusi yamuunga mkono Saif Gaddafi urais Libya

MOSCOW, URUSI

SERIKALI za Urusi na Italia kwa nyakati tofauti wiki hii zimeunga mkono uwezekano wa mtoto wa aliyekuwa Kiongozi wa zamani wa Libya, Saif al-Islam Gaddafi kurudi katika siasa na kuwania urais.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Mikhail Bogdanov alisema mwana huyo wa marehemu Kanali Muammar Gaddafi anapaswa kushiriki kikamilifu katika siasa ili kurejesha taifa hilo katika mstali.

Kauli ya Urusi inakuja baada ya vyombo vya habari vya Urusi kuchapisha taarifa kuwa mmoja wa wawakilishi wa Saif aliwasilisha barua kwa Moscow mapema mwezi huu kuomba msaada ili kusafisha njia ya kurudi kikamilifu katika siasa.

Mataifa ya Magharibi na Umoja wa Mataifa yanalishinikiza taifa hili la Kaskazini mwa Afrika kufanya chaguzi mwaka ujao ili kujaribu kumaliza miaka saba ya ukosefu wa utulivu katika taifa hilo mzalishaji wa mafuta.

Baba wa Saif aling’olewa na kuuawa katika mapinduzi ya mwaka 2011, ambayo yalishuhudia Saif akikamatwa na kuwekwa jela kwa miaka kadhaa kabla ya kuachiwa hivi karibuni.

Saif alikuwa akionwa kama mtu mwenye mtazamo wa kimageuzi, anayefaa kumrithi baba yake kabla ya mwaka 2011 na amebakia kama mtu muhimu kwa wafuasi wa Gaddafi.

“Tunamuunga mkono kila mtu na tunaamini hakuna mtu anayepaswa kutengwa katika jukumu la ujenzi wa taifa kisiasa,” Bogdanov alikaririwa akisema.

“Ndiyo maana trunawasiliana na makundi yote yaliyopo magharibi, mashariki na kusini mwa nchi. Saif al-Islam anaungwa mkono na makabila katika maeneo fulani ya Libya na hivyo anastahili kushiriki kikamilifu kisiasa kwa ujenzi wa nchi yake.”

Wakati huo huo, Italia mshirika wa zamani wa Gaddafi imesema haina tatizo na kuibuka kwa Saif kuelekea urais wa Libya iwapo atashinda uchaguzi kidemokrasia.

Katibu wa Baraza la Mawaziri Italia, Giancarlo Giorgetti alisema taarifa kuhusu kurudi kisiasa kwa mtoto huyo wa pili wa Gaddafi ni kitu ambacho ni ngumu kukitathimini kutokana na hali ya kisiasa ilivyo kwa sasa.

“Lakini iwapo watu wanamkubali kuwa kiongozi wao kwa mchakato wa kidemokrasia, ni haki yake na yao kwa sababu hii ndiyo demokrasia,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles