29.1 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

URUSI YAISHUTUMU MAREKANI KUIVURUGA SYRIA

MOSCOW, URUSI


WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameishutumu Marekani kwa kuivuruga makusudi Syria baada ya kukusanya jeshi la waasi na kuwapatia mafunzo na silaha hali ikijua kuna Serikali.

Lavrov amesema kitendo cha Marekani kuunda kikosi cha kijeshi mipakani mwa Syria, kitasababisha taifa hilo kugawanyika katika maeneo.

“Hatuoni juhudi za kusaidia kuutatua mzozo huu haraka iwezekanavyo, bali za kuwasaidia wale wanaotaka kuchukua hatua za kubadilisha utawala wa Jamhuri ya Kiarabu ya Syria.

“Marekani inafahamu inaowasaidia wanapigana kinyume na Serikali halali ya Syria na hivyo malengo yake ni kuigawa nchi pamoja na kutaka kuuondoa uongozi halali wa Rais Bashir al Assad,” alisema Lavrov.

Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa Syria, ikiwa pamoja na Iran, zimekuwa zikiisaidia Serikali ya Assad kukabiliana na makundi ya waasi yanaoungwa mkono na Magharibi.

Kauli ya Lavrov inakuja baada ya Jeshi la Marekani na washirika wake kushirikiana na wapiganaji wa Syria kuweka kikosi kipya cha askari 3,000, hatua ambayo pia imeikasirisha Uturuki.

Hasira ya Uturuki ni kutokana na msaada huo kulenga kuwasaidia wanajeshi wa Kikurdi nchini Syria, ambao pia inapambana nao.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Uturuki, ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa mafunzo ya Marekani yanayotolewa kwa kikosi cha ulinzi wa mpakani, ndiyo sababu iliyofanya balozi mdogo wa Marekani kuitwa mjini Ankara Jumatano wiki iliyopita.

Marekani imepanga kuviweka vikosi hivyo baada ya kufuzu mafunzo kwenye mipaka ya eneo linalodhibitiwa na Wapiganaji wa Jeshi la Demokrasia Syria (SDF), kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo, ambako kunadhibitiwa na Wakurd.

Mipaka hiyo inapakana na Uturuki na Irak katika upande wa kusini mashariki, na kwenye Bonde la Mto Euphrates, ambao ni mstari unaotenganisha wanajeshi wa SDF wanaoungwa mkono na Marekani na wale wa Serikali ya Syria wanaoungwa mkono na Iran na Urusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles