MOSCOW, Russia
BIASHARA kati ya nchi za Russia na Ujerumani inaripotiwa kuimarika zaidi katika kipindi cha mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana. Hayo yamesemwa na Rais wa Russia, Vladimir Putin, katika mkutano wake na wafanyabiashara wa Kijerumani wanaondesha shughuli za uwekezaji nchini humo.
Rais huyo alisema kuwa kwa mwaka huu katika uwekezaji huo baina ya nchi hizo mbili umeweza kuongeza pato la asilimia 25. Kiongozi huyo alisema kuwa katika kipindi cha mwaka jana mauzo ya biashara yalifikia dola bilioni 40.7 wakati uwekezaji wa moja kwa moja uliofanywa na makampuni ya Ujerumani katika uchumi wa Urusi yalifikia dola bilioni 18.
Alisema katika kipindi cha mwaka huu biashara baina ya nchi hizo mbili ilikuwa kwa asilimia 25 na uwekezaji katika robo ya kwanza peke yake ilifikia dola bilioni 312, ikilinganishwa na mwaka jana katika kipindi kama hicho kiasi cha uwekezaji zilikuwa ni dola bilioni 225.
“Zaidi ya kampuni 5,000 za Kijerumani ambazo zinaendesha shughuli zake nchini hapa, pia zimeweza kuajiri raia 270,000 na mauzo ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hizo yameongezeka kwa dola bilioni 50,” alisema Rais Putin.