MOSCOW, Urusi
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, ameelezea kwa kina kuhusu uhusiano baina ya nchi yake na Armenia zinavyoshirikiana katika nyanja mbalimbali, zikiwamo za kisiasa na kiuchumi.
Rais Putin aliyasema hayo juzi, wakati akizungumza na Rais wa Armenia, Serzh Sargsyan, ambaye alikuwa nchini hapa kwa ziara ya kikazi.
Akizungumza na kiongozi huyo, Putin alisema kwa nchi yake, bado inaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano ambayo yalifikiwa wakati Rais Sargsyan alipokuja nchini hapa mapema machi, mwaka huu.
“Ningependa kutambua kwamba, timu zetu zote hufanya kazi kwa bidii juu ya utekelezaji wa mikataba yetu iliyofikiwa wakati ulipotembelea Urusi Machi mwaka huu. Mafanikio haya ni matokeo ya ushirikiano wetu katika nyanja za mawasiliano, kisiasa, usalama na uchumi,” alisema Rais Putin, katika mazungumzo na rais mwenzake huyo.
Ukuaji wa uchumi ulikuwa umeanza kukua tangu mwaka jana na mwaka huu takwimu tayari zinaonesha ongezeko, jambo ambalo alidai ni kufurahisha na kwamba angependa hali hii inaendelea.
Kiongozi huyo wa Urusi alifafanua pia mbali na mafanikio hayo, pia ushirikiano wao katika masuala ya utamaduni na misaada ya kibinadamu nao unaendelea kukua kwa haraka.