24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

RUTO AMLAUMU RAILA

NAIROBI, KENYA

NAIBU Rais wa Kenya, William Ruto, amemtaja Raila Odinga kama mwanasiasa asiye na demokrasia na mshamba kutokana na vurugu na ghasia zilizoshuhudiwa jijini alipopokelewa na wafuasi wake waliofurika katika barabara za jijini hapa  kumkaribisha kiongozi wao, lakini wakakabiliana na polisi waliokuwa wakiwazuia kufika kwenye bustani ya Uhuru ambako walipanga kuandaa mkutano mkubwa wa kisiasa.

Akizungumzia hatua ya Jeshi la Polisi kuwasambaratisha wafuasi wake, Raila alilalamikia vitendo vya polisi kwa wafuasi wake na viongozi wa NASA, akishangazwa kwa nini viongozi hao wawili hawakuja kwenye uwanja wa ndege kukutana naye alipowasili kutoka Marekani.

“Mmenisubiri kutoka asubuhi na ninasema asante. Mmeonyesha upendo mkubwa. Hasira yangu ni kwa huyu kijana mdogo Uhuru Kenyatta. Badala ya kuja kunikaribisha kwenye uwanja wa ndege, aliamua kukaa na naibu wake,” Raila alisema.

Wakati msafara wa Raila ulipokuwa ukiingia jijini kwa takriban saa sita, magari kadhaa yaliharibiwa kwenye makabiliano hayo huku polisi wakitumia vitoa machozi, mawe na risasi kamili kuwazuia viongozi wa upinzani na wafuasi wao kufika jijini.

Watu watano walipoteza maisha yao, huku wengine wengi wakipata majeraha tofauti kwenye makabiliano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles