29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Upinzani washinikiza Rais Keita ajiuzulu

 BAMAKO, MALI

WAPINZANI nchini Mali wameendelea kung’ang’ania msimamo wao wa kutaka kujiuzulu Rais wa nchi hiyo, Ibrahim Keita huku kukifanyika juhudi za kieneo na kimataifa za kujaribu kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Viongozi wa upinzani nchini Mali chini ya mwavuli wa Harakati ya Juni 5 wamesisitiza kuwa, Rais Keita anapaswa kujiuzulu, Bunge livunje na kisha kuundwe serikali ya muda.

Juzi wapinzani hao walikutana na ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (Ecowas) kama moja ya juhudi za kutaka kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

Wajumbe wa jumuiya hiyo ya kikanda walitoa mapendekezo kadhaa kwa upinzani hasa kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itaanzisha mageuzi ya kisiasa na mashtaka dhidi ya wahusika wa mauaji ya raia waliouawa wakati wa maandamano.

Hata kama upinzani nchini Mali unadai kwamba utatoa majibu yake rasmi kwa mapendekezo yaliyotolewa baada ya mkutano wao usiokuwa wa kawaida, lakini tayari baadhi yao wameonyesha kupinga mapendekezo hayo.

Mgogoro wa kisiasa nchini Mali ambao uliibuka baada ya kufanyika uchaguzi wa Bunge mnamo Machi mwaka huu, umezusha wasiwasi mkubwa si tu ndani ya nchi hiyo, bali pia katika nchi jirani na nchi hiyo.

 Wiki iliyopita, Rais Keita alisema kuwa, anakaribisha hatua ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, kubadilisha wajumbe wa Mahakama Kuu na kulivunja Bunge. Hata hivyo wapinzani wake wamesema hatua hizo hazitoshi kwani wanachotaka wao na Rais Keita kuondoka madarakani.

Hata hatua ya hivi karibuni ya Rais Keita ya kuvunja Mahakama ya Katiba nayo haijasaidia kuwatuliza wapinzani ambao wameendelea kutoa wito wa kuendelezwa maandamanao na uasi wa kiraia hadi rais huyo atakapoaondika madarakani.

AP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles