30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

UPENDO MLAY KUIPAISHA SANAA YA ‘MAKE UP’

NA JUMA3TATA RIPOTA


UKIACHA sanaa za muziki na filamu ambazo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na tija kwa wasanii, jamii na Taifa kwa ujumla, sanaa ya mitindo na upambaji (Make Up) nayo inakuja juu kwa kasi.

‘Make Up’ imekuwa na umuhimu mkubwa kwa wasanii wa muziki na filamu pale wanapotaka kusimama mbele ya mashabiki wao na mara nyingi sanaa hii hutumika kuwapendezesha maharusi.

Juma3tata leo tumefanya mazungumzo na msanii wa ‘Make Up’, Upendo Mlay kutoka jijini Arusha ambaye ukubwa wa kazi zake umefanya aingie kwenye tuzo za Swahili Fashion Week (SFW 2017) zitakazotolewa mwezi ujao, karibu

JUMA3TATA: Mashabiki wanapenda kujua una muda gani kwenye sanaa hii?

Upendo Mlay: Nilikuwa napenda urembo na mitindo toka nikiwa mtoto ila nilianza kujishughulisha na sanaa ya ‘Make Up’ mwaka 2015 na rasmi kabisa ilikuwa mwaka 2016, ambapo nahusika zaidi kuwapamba maharusi pamoja na pia nafanya sanaa ya mitindo (Fashion).

JUMA3TATA: Changamoto zipi unakutana nazo kwenye sanaa yako?

Upendo Mlay: Changamoto ni nyingi japokuwa zinatatulika ila kubwa zaidi ni kufanya kazi na wateja ambao wameshapata ‘stress’ kabla ya kufika kwangu hasa maharusi ambao wamechelewa kufika na wanataka kuwahi kwenda kufunga ndoa.

JUMA3TATA: Mipango yako ni ipi ili kuhakikisha unatanua wigo wa sanaa yako?

Upendo Mlay: Mipango ipo mingi ila kwasasa naona kama ni mapema mno kuiweka hadharani ila watu watarajie mambo mazuri kutoka kwangu, ndiyo maana kwa muda mfupi niliofanya sanaa ya ‘Make Up’ tayari nimeingia kwenye tuzo..

JUMA3TATA: Tumeona umeingia kwenye tuzo za Swahili Fashion Week, hii ni mara yako ya ngapi?

Upendo Mlay: Hii ni mara ya tatu kuingia, mwaka 2015 niliipata tuzo ya Mwanamitindo Bora wa Mwaka (Model Of The Year) kipindi hicho nilikuwa nimejikita zaidi kwenye masuala ya mitindo. Mwaka jana pia nikaingia kwenye kipengele cha Msanii wa Make Up wa Mwaka (Make Upe Artist Of The Year) hali kadharika mwaka huu.

JUMA3TATA: Je tasnia ya filamu inawatumia ipasavyo wasanii kama nyinyi ili kuleta uhalisia wa vitu kama majeraha, vidonda nk katika fiamu zao?

Upendo Mlay: Bado hatutumiki ipasavyo kwa kuwa wasanii wengi wa ‘Make Up’ hawana ndoto kubwa wanawaza kuishia kuwapamba maharusi tu, lakini upande wangu mipango ya kufanya mapinduzi ya ‘Make Up’ kwenye filamu ipo kwa kuwa ni ndoto zangu.

JUMA3TATA: Mashabiki wanaweza kukupigia vipi kura kwenye tuzo za SFW?

Upendo Mlay: Unaweza kunipigia kura kwa jina mbili. Njia ya kwanza ni njia ya meseji kwa kuandika neno SFM MA 07 na kuituma kwenda namba 15670.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles