24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

UNFPA yaomba ushirikiano

kwayuNa MWANDISHI WETU, SHINYANGA

USHIRIKIANO kati ya jamii na viongozi, unahitajika ili kuweza kudhibiti ongezeko la idadi ya ndoa na mimba za utotoni.

Hayo yameelezwa juzi na Msaidizi wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA) nchini, Christine Kwayu, alipokuwa akizunguza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani.

“Kama juhudi za kudhibiti ongezeko hilo hazitafanywa, UNFPA inakadiria kuwa, miaka 10 ijayo jumla ya wasichana milioni moja walio chini ya umri wa miaka 18 watakuwa wameolewa.

“Jamii inapaswa kuelimishwa kuwa mtoto wa kike ana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo Tanzania, lakini hilo halitaweza kufikiwa kama hatutawathamini watoto hawa,” alisema Kwayu.

“Ili kuhakikisha mtoto wa kike anathaminiwa, UNFPA inafanya kazi kwa ukaribu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kwa kuwa ofisi hizo zinahusika na masuala hayo.

“Takwimu za NBS zinaonyesha Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni kwa asilimia 59 ukifuatiwa na Tabora wenye asilimia 58, Mara asilimia 55, Dodoma 51, Lindi 48, Mbeya 45, Morogoro 42, Singida 42, Rukwa 40 na Ruvuma una asilimia 39.

“Mikoa mingine yenye idadi kubwa ya ndoa za utotoni ni Mwanza 37, Kagera 36, Mtwara 35, Manyara 34, Pwani 33, Tanga 29, Arusha 27, Kilimanjaro 27, Kigoma 29, Dar es Salaam 19 na Iringa asilimia nane.

“Takwimu zinaonesha asilimia 42 ya wasichana barani Afrika, huolewa wakiwa na umri wa chini ya miaka 18 na suala hili si la kufumbiwa macho kwa sababu halikubariki,” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, alisema Serikali haitazivumilia mila potofu ikiwamo kuwapeleka watoto wa kike kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kuwaondoa mikosi ili wapendwe na wanaume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles