23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

UNFPA yaikabidhi Serikali vifaa vya afya vyenye thamani ya dola milioni 4.5

*Vitasaidia kuokoa maisha ya uzazi
*Vimejumhisha vifaa vya uzazi wa mpango vya kisasa

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Katika kuhakikisha kuwa wanawake, wanaume na vijana wanapata huduma bora za uzazi wa mpango, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na mpango wa uzazi(UNFPA) limekabidhi kwa Serikali vifaa vya kuokoa maisha ya uzazi vikiwemo vifaa vya kisasa vya uzazi wa mpango.

Kwa mujibu wa UNFPA vifaa hivyo vinathamani ya dola za Marekeni milioni 4.5, aidha kwa mwaka 2022 ambapo kati ya fedha hizo Dola milioni 4 nikutoka UNFPA na dola 500,000 ni kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Kimataifa na Jumuiya ya Madola ya Uingereza(FCDO).

Akizungumza wakati wa Makabidhiano hayo ambayo yamefanyika leo Jumatatu Julai 18, 2022 Bohari Kuu ya Dawa(MSD) Keko Dar es Salaam, Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner amesema vifaa hivyo vitasidia watu binafsi kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya afya zao za uzazi, pindi na wakati sahihi wa kupata watoto.

“Kama ilivyokaulimbiu yetu kwamba; “Kila ujauzito unahitajika na kila uzazi ni Salaam,” hili ndilo dhumuni letu la kutambua lengo letu la pamoja la kuhakikisha kuwa wanawake, wanaume na vijana wote nchini Tanzania wanapata bidhaa za uzazi wa mpango, bila kumuacha mtu nyuma.

“Vifaa hivi vinatoa njia za uwezeshaji binafsi, hasa kwa wanawake na wasichana. Lengo letu la pamoja ni usambazaji wa dawa hizi za uzazi wa mpango na vifaa vya afya ya uzazi kwa maelfu ya vituo vya afya, hospitali, zahanati na huduma za kijamii, kisha kusambazwa ili kutoa haki na chaguo za upangaji uzazi kwa wanawake na wanaume kote nchini.

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa dhamira ya FP2030 ya kuendeleza uzazi wa mpango unaozingatia haki na ongezeko lililopangwa la 10% la kila mwaka katika mgao wa sasa wa Sh bilioni 14 za Tanzania zitakazotolewa kikamilifu kwa ajili ya ununuzi wa vidhibiti mimba,” amesema Mark na kuongeza kuwa:

“Kupitia ushirikiano wa UNFPA wa Ugavi, tunatazamia kushirikiana zaidi na Tanzania mwaka huu ili kuanzisha maelewano ya nchi na kuimarisha dhamira yetu ya pamoja ya ufadhili wa siku zijazo kwa ajili ya vifaa vya afya ya uzazi. Hii ni hatua muhimu na endelevu wa uzazi wa mpango nchini Tanzania,” amesema Mark.

Sehemu ya vifaa hivyo.

Amesema kuanzia Mwaka 2015 hadi 2021 UNFPA na FCDO zimenunua 53% ya vifaa vya afya ya uzazi nchini Tanzania.

“Jumla ya thamani ya bidhaa hizi ji dola milioni 54.2 ambapo zaidi ya milioni 24.8 zilitolewa na FCDO na milioni 29.4 zilitolewa na UNFPA.

“Vifaa hivi zilitoa vidhibiti mimba vya kutosha vya kisasa kutosheleza mahitaji ya wanandoa milioni 21 kwa mwaka mmoja.

“Tunakadiria bidhaa hizi zitapunguza mimba zisizotarajiwa milioni 9, kuzuia vifo vya karibu milioni moja vya uzazi, kuzuia utoaji mimba usio salama milioni 2 na kuokoa dola za Marekani milioni 756 katika huduma ya moja kwa moja ya afya.

“UNFPA inaunga mkono serikali ya Tanzania kutimiza ahahdi ya mkutano mkuu wa Nairobi mwaka 2019 wa kusaidia upatikanajiwa afya ya uzazi, watoto wachanga na vijana.

“Tunalenga kuhakikisha kuwa hakuna anayeachwa nyuma wakiwamo watu wenye ulemavu wakimbizi na wale welio hatarini zaidi,”amesema Mark.

Akipokea vifaa hivyo Mratibu wa Afya ya Mtoto Wizara ya Afya na Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Uzazi, Dk. Felix Bundala amepongeza UNFPA kwa msaada huo na kusama kuwa hiyo itawezesha Watanzania kuwa na uzazi salama ikiwamo kuokoa vifo vinavyotokea wakati na baada ya kujifungua.

“Awali, tulikuwa na changamoto hii ya ukosefu wa vifaa vya afya ya uzazi salama, hivyo jukumu letu sasa ni kuhakikisha kuwa tunasambaza vifaa hivi ili viweze kufika kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner(kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi ofisi ya Maendeleo ya Uingereza, kimataifa na Jumuiya ya Madola, Kemi Williams wakati wa kukabidhi vifaa hivyo leo Julai 18, 2022 Keko jijini Dar es Salaam.

“Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata fursa ya kupanga uzazi bora na salama na kuona kuwa hakuna mtoto anayepoteza maisha au anayezaliwa nje ya mipango ya wazazi,” amesema Dk. Bundala.

Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai amesema watavitunza vifaa hivyo na kuhakikisha kuwa vinafika kwenye maeneo yote yaliyolengwa nchini.

“Lengo letu kama Bohari ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kuimarisha mfumo wa ugavi pia kuweka vifaa hivi kwenye mazingira salama,” amesema Tukai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles