TAASISI inayojishughulisha na watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism), Under the Same Sun, kwa kushirikiana na Chuo cha Filamu nchini Sweden (Swedish Film Institute) zipo katika mpango wa kutayarisha filamu ya elimu juu ya watu hao na mauaji dhidi yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Vicky Nketema, alisema wanaamini kupitia mpango huo utatoa ujumbe wa kupunguza mauaji ya albino yaliyowahi kushika chati nchini.
“Tumeamua kutumia njia hii ya filamu kwa kuwa tunaamini itakuwa rahisi kufikisha elimu kwa jamii ili kusaidia uelewa juu ya albino na maisha yetu kwa ujumla,” alisema.
Filamu hiyo inayoandaliwa na kuongozwa na watu kutoka nje ya Tanzania na kuchezwa na waigizaji wa Tanzania ina jina la ‘The Inner Struggle’.