25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 9, 2024

Contact us: [email protected]

UMEME WA SOLA UNAVYOMPA HESHIMA AKON BARANI AFRIKA

Na BADI MCHOMOLO

RAPA Aliaume Thiam ‘Akon’ raia wa nchini Senegal, amekuwa kimya sana kwenye muziki kwa kipindi cha hivi karibuni tofauto na miaka ya 2002.

Kuna kipindi msanii huyo alikuwa miongoni mwa wasanii wa hip hop nchini Marekani kushirikishwa kwenye nyimbo mbalimbali za wasanii wenzake, hivyo alizidi kujitengenezea jina kubwa.

Kutokana na aina ya sauti yake aliweza kuwateka mashabiki wengi ndani ya nje ya Marekani hasa kutokana na wimbo wake wa ‘Blame It On Me’ Don’t Matter ambapo nyimbo hizo aliziachia 2006, pamoja na zingine nyingi.

Watu wengi wa muziki walimuelewa sana msanii huyo kutokana na ngoma zake kali, na walishangaa kuona anafanya vizuri nchini Marekani wakati yeye ni raia wa nchini Senegal, lakini jibu lake lilikuwa jepesi kwamba alikuwa mwepesi wa kutamka maneno ya ndani zaidi kwa ufasaha.

Akon alitambua kwamba kwa bara la Afrika ambalo ni masikini kuna idadi kubwa ya watu ambao hawamjui labda kwa kuwa sio wapenzi wa muziki.

Hivyo aliamua kufungua kampuni yake ambayo inajulikana kwa jina la ‘Akon Lighting Africa’ akiwa na lengo la kutokomeza tatizo la umeme Afrika.

Msanii huyo alikulia katika mkoa wa Kaolack nchini Senegal, ambapo mkoa huo ulikuwa miongoni mwa ile ambayo ina tatizo la umeme, hivyo baada ya kufanya vizuri kwenye muziki aliona bora asaidie umeme Afrika.

Kampuni ya Akon Lighting Africa, aliianzisha Februari 2014, ambapo hadi sasa amefanikiwa kuwaajiri zaidi ya wafanya kazi 5,000.

Lengo laki ni kusambaza umeme wa sola kwa nchi 14 za barani Afrika, na hadi sasa tayari amesaidia katika vijiji vya nchini Senegal, Guinea, Mali, Benin na Sierra Leone.

Wiki iliopita timu nzima ya Akon Lighting Africa, ilikuwa nchini Gambia kwenye kijiji cha Sareh Patch, ambacho kina wakazi zaidi ya 4,000 wasio na umeme, hivyo baada ya siku chache watakuwa wanafurahia maisha ya kisasa kwa kila nyumba kuwa na umeme.

Mbali na hapo, baadhi ya wanakijiji wa nchini Cape Verde, tayari wameanza kunufaika na mpango huo baada ya kusambaziwa umeme na kampuni hiyo.

“Nitapambana kuhakikisha sehemu kubwa ya Afrika inapata umeme wa sola kwa zile nchi 14 ambazo, ninaamini tayari kuna sehemu wananufaika na umeme huo na sehemu zingine tunaendelea kutoa huduma hiyo,” alieleza Akon

Kwa hali ya kawaida Akon kwa sasa amezidi kulitangaza jina lake hadi kwa wale ambao walikuwa hawapendi muziki, lakini kwa sasa watakuwa wanamjua na kumuona kama mfalme kule vijijini kupitia umeme wake.

Leo hii msanii huyo anaonekana kuwa kimya na baadhi ya mashabiki wake kujiuliza kuwa yupo wapi kwa sasa, kumbe kuna wengine kama vile Gambia, Cape Verde, Guinea, Mali na nchi zingine ndio kwanza wanasikiliza nyimbo zake kupitia umeme aliowawekea.

Atakuwa na heshima kubwa kwenye nchi hizo kutokana na jambo analolifanya, wapo ambao wanaona kuwa msanii huyo ni zaidi ya mfalme.

Umeme ni sehemu moja wapo ya kupiga hatua kimaendeleo ya uchumi ndani ya Taifa.

Kuna baadhi ya watu maarufu barani Afrika hasa wachezaji wa soka wamekuwa wakitoa huduma kwa jamii kama vile mchezaji wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba, ambaye amefungua hospitalia zake tano nchini humo, huku Samuel Eto’o akiwa na mtandao wake wa simu nchini Cameroon ukijulikana kwa jina la Set’Mobile

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles